.Mafuta yamepanda Bei Cha ajabu nauli ipo palepale hii kwetu ni hasara na haitulipi

Na.Vero Ignatus,Arusha

Wakazi wa  Baadhi ya maeneo, wamalelazimika kutembea kwa miguu,na wengine kukodi bajani na bodaboda  baada ya madereva wa daladala kugoma kutoa huduma ya usafiri ,kwa kile wanachoekezea kua ni kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta

Akizungumza na Michuzi Blog asubuhi ya leo Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Justine Masejo  amesema kuwa wapo wanaendelea kutumia Busara,katika kuangalia namna ya kuitatua changamoto hiyo kwa kushirikiana na Latra

Anasema William Emmanuel dereva daladala:Kilio chetu ni mafuta yamepanda Bei ipo palepale na imepungua kuliko Ile ya zamani, Serikali ilifanyie jambo hili kazi haraka kwani kila siku mafuta yamepanda.

"Kwa mujibu wa Viongozi wetu mtu anayeona inamliapa basi  anaweza kufanya kazi, na wote wameona haiwalipi  dereva USA kikatiti Maoni yangu waongeze nauli tengeru 500-700 USA 700-1000 Kikatiti 1200, Serikali ikitoa neno Abiria watatoa nauli .anasema Charles  kondakta wa daladala ruti ya tengeru- Kikatiti

Mgomo huu tulikuwa hatujauweka ni kutokana na mafuta kuoanda 2836-3321 nauli ni ileile kwenda tengeru USA- kikatiti ukiweka mafuta hailipi kabisa Stivin Kessy Dereva

Kwa upande wake Katibu wa daladala Elias Hassan mkoa wa Arusha amesema kwa Sasa juhudi zinafanyika kuwaomba madereva hao kurudi barabarani ili kuwasaidia wananchi huku wao wakiendelea na kikao Cha namna tatizo hilo litatatuliwa

"Tupo tunaingia kwenye kikao tuone namna ya kupata maridhiano kwa madereva kuepusha usumbufu kwa Abiria"amesema Elias

"Wenzetu daladala wamegoma kwetu sisi Bajaji ni fursa na tunaitumia ili kuwarahisushia wananchi kuendelea na shughuli zao wasikwame"anasema dereva babaji kwa sharti la kutotajwa Jina lake

"Tunawapeleka kwa Mrombo kwa sh 1000 kwa hiyari yao wenyewe kwa anayehitaji usafiri"alisema dereva huyo.

Eneo hili huwa yanapaki daladala za kwenda kisongo kwa mworombo na sehemu nyingine Kama linavyoonekana pako wazi hakuna daladala wamegoma, yanaonekana magari yawatu binafsi yameegeshwa.Picha na Vero Ignatus.
Eneo hili huwa yanapaki daladala za kwenda Ngaramtoni Tengeru USA kikatiti na kwingineko,Kama inavyoonekana pako wazi hakuna daladala wamegoma Picha
Baadhi ya Madereva  wa daladala wa ruti mbalimbali JiJini Arusha wakiwa wamekaa ndani ya gari wakisema hakuna kazi leo.Picha na Vero Ignatus
Abiria wakiwa katika moja ya kituo wakisubiria walau Kama watapata usafiri
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...