Maafisa Jenerali.Wakuu wa Matawi MMJWakuu wa Idara na Vitengo.Kamati Kuu

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb), ameainisha vipaumbele vya Wizara wakati anawasilisha Bungeni Hotuba ya Wizara kuhusu makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 tarehe 19 Mei, 2022.

Amesema Mwelekeo wa shughuli zinazokusudiwa kufanyika katika Mwaka wa Fedha 2022/2023 utazingatia maeneo ya kipaumbele yakiwemo; Kuliimarisha Jeshi kwa kulipatia zana na vifaa vya kisasa, mawasiliano, rasilimali watu pamoja na kutoa mafunzo, Kuweka mazingira mazuri ya utendaji kazi wa Jeshi ikiwemo mafunzo, Kuendeleza jitihada za utatuzi wa changamoto za mipaka ya nchi yetu na nchi jirani; Kuboresha mazingira ya kazi, makazi na kuimarisha upatikanaji wa huduma stahiki na Kuendelea kujenga uwezo wa Jeshi la Kujenga Taifa kwa zana na vifaa vya kilimo ili liweze kujitosheleza kwa chakula na kuboresha miundombinu katika vikosi ili liweze kuchukua vijana wengi zaidi.

Maeneo mengine aliyoyainisha ni pamoja na Kuendeleza tafiti na uhuwilishaji wa teknolojia kwa ajili ya kuzalisha bidhaa na huduma kwa matumizi ya kijeshi na kiraia; Kuimarisha na kuratibu Mafunzo ya Jeshi la Akiba, Kuimarisha ushirikiano na Jumuiya za Kimataifa, Kikanda na nchi moja moja katika nyanja za kijeshi na kiulinzi, Kuendelea kushirikiana na Mamlaka za Kiraia kukabiliana na majanga na dharura; na Kufanya upimaji, uthamini na ulipaji fidia ya ardhi katika maeneo yaliyotwaliwa kwa ajili ya matumizi ya Jeshi.

Akiwasilisha Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ulinzi na JKT kwa Mwaka wa Fedha 2022/23, amesema Serikali inatarajia kutenga fedha shilingi Tilioni 2.7 kwa ajili ya fedha za matumizi ya kawaida na maendeleo.

Ambapo Shilingi Tilioni 2.4 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Shilingi bilioni 340 ni kwa ajili ya kugharamia shughuli za maendeleo. Ongezeko ni Shilingi Bilioni 335.

Mwelekeo kwa mwaka ujao wa fedha 2022/2023, Dkt. Stergomena amebainisha kuwa Wizara yake kwa kuzingatia Dira na Dhima ya Wizara, Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, mppango wa Tatu wa Maendeleo wa miaka Mitano 2021/22 – 2025/26), Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030(SDGs), Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi na Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango wa Bajeti ya Seilali kwa Mwaka wa edha 2022/2023.

Aidha, Mheshimiwa Dkt Stergomena amewasilisha Mapitio ya utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2021/22 ambapo Wizara iliidhinishiwa Jumla ya shilingi Tilioni 2.4 kwa ajili ya Matumizi ya kawaida na maendeleo katika mafungu yake matatu (Wizara, NGOME na JKT). Kati ya fedha hizo Shilingi Bilioni 2.2 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Shilingi bilioni 176.6 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

Kwa Mwaka wa Fedha 2022/23 Wizara imefanikiwa kutekeleza shughuli mbalimbali kwa kutumia Fedha zilizotolewa kwa ajili ya matumizi ya kawaida na maendeleo. Shughuli zilizotekelezwa ni pamoja na mafunzo ya kijeshi, mafunzo ya Jeshi la Akiba, huduma za afya na tiba, ushirikiano wa kiulinzi na kijeshi na nchi nyingine, ushirikiano na mamlaka za kiraia katika shughuli mbalimbali za kitaifa, mafunzo ya vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa, mapambano dhidi ya magonjwa ambukizi na yasiyoambukiza, utawala bora na utunzaji mazingira.

Kwa upande wa fedha za maendeleo baadhi ya shughuli zilizotekelezwa ni pamoja na ununuzi wa zana na vifaa, uboreshaji wa zana za ulinzi wa anga, ujenzi wa mahanga ya kuhifadhia ndege na zana, kuboresha miundombinu ya majengo hospitali ya kanda ya mwanza, kugharamia mradi wa mawasiliano salama jeshini na kutatua migogoro ya ardhi kwa kupima, kufanya uthamini, na kulipa fidia, ununuzi wa magari ya Makamnda na Waambata Jeshi na kuendeleza Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa.

Kuhusu hali ya ulinzi na usalama wa mipaka ya nchi,Dkt. Stergomena amesema katika Mwaka huu wa Fedha hali ya mipaka ya nchi yetu yenye urefu wa jumla ya kilomita 5,461.20 ianyohusisha eneo la nchi kavu na majini, imeendelea kuwa shwari. Katika kipindi hicho hapakuwa na matukio ya uhasamayaliyoripotiwa baina yetu na nchi tunazopakana nazo, licha ya kuwepo kwa changamoto kadhaa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...