Benki
ya Equity (T) leo Jumatano imezindua rasmi tawi lake jipya wilaya ya
Kahama mkoani Shinyanga. Tawi hili lipo Kahama mjini jengo la MACHALI
TOWER na huduma zote za kibenki zitakuwa zinapatikana kuanzia siku ya
jumatatu mpaka jumamosi. Hatua hii ni moja ya muendelezo wa benki
kuongeza wigo wake wa upatikanaji nchini ili kuweza kuwafikia wateja
wote Tanzania na kuhakikisha kuwa tunatimiza dhamira yetu ya kubadilisha
maisha ya kila Mtanzania. Uzinduzi huu umefanywa na mkuu wa wilaya ya
Kahama ndugu Festo Kiswaga ukishuhudiwa na baadhi ya wageni waalikwa.
Akizungumza katika hafla ya
uzinduzi wa tawi hilo, mkuu wa wilaya alisema, “Hatua hii itatuongezea
wigo wa mtandao wa utoaji huduma zetu ambazo ni nafuu zaidi nchini na
hivyo kuendana na lengo letu la kukomboa Watanzania kiuchumi kwa
kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anatumia mifumo rasmi ya kifedha
(financial inclusion).
Pia msemaji wa benki alisema
“Akaunti zetu hazina makato ya mwezi na tuna viwango bora kabisa vya
riba sokoni. Pia kupitia tawi hili huduma nyingi zitatolewa ikiwemo
kufungua akaunti na kupata mikopo mbalimbali” amesema Betty Kwoko.
Kuhusu Benki ya Equity
Equity Bank (T) ni Benki yenye
matawi 15 nchini ikiwa na zaidi ya wafanyakazi 1200 ukiwa ni moja ya
uwekezaji mkubwa zaidi ulioanzia nchini Kenya na baadaye kusambaa katika
nchi nyingine za Afrika ikiwemo Tanzania, Uganda, Ethiopia, Congo-DRC,
Rwanda na Sudan ya Kusini. Kwa maelezo zaidi: grace.majige@equitybank.co.tz, 0688988110.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...