Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amesema kuwa, uhalifu nchini umeendelea kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na jitihada mbalimbali na ushirikiano wa vyombo vya ulinzi na usalama, vikundi vya ulinzi shirikishi pamoja na wananchi.
IGP Sirro amesema hayo akiwa wilaya ya Urambo na Kaliua mkoani Tabora ambapo pia ameelezea changamoto za mauaji ya ushirikina na kuwataka wananchi kuachana na imani potofu na zilizopitwa na wakati na kwamba Jeshi la Polisi litaendelea kuwachukulia hatua kali watu wote wanaojihusisha na vitendo hivyo.
Aidha IGP Sirro amevitaka vikundi vya ulinzi shirikishi kuzingatia sheria na kuwahudumia wananchi badala ya kuwa kero kwa wananchi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...