CHAMA
Cha Mapinduzi (CCM) kimepiga marufuku wagombea nafasi za uongozi ndani
ya Chama hicho nchi nzima ambao ni viongozi kutojihusisha kwenye kutoa
fomu za kugombea uongozi au kusimamia Uchaguzi.
Kimesema iwapo
kiongozi kwenye nafasi yoyote anagombea nafasi ndani ya Chama hicho ni
vema Chama kikateua mtu mwingine wa kusimamia ili kuhakikisha haki
inatendeka katika mchakato wa Uchaguzi unaoendelea nchi nzima.
Hayo
yamesemwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo
alipokuwa kwenye ziara yake mkoani Shinyanga ambapo amezungumzia umuhimu
wa kutenda haki kwenye mchakato huo wa Uchaguzi.
Amefafanua
kwamba mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi ndani ya chama, hivyo wagombea
ambao kwa sasa ni viongozi ngazi zote hawapaswi kusimamia uchaguzi ili
hali wao ni sehemu ya wagombea na kutaka wakae pembeni kuanzia mchakato
wa awali wa ugawaji wa fomu, mpaka vikao vya kupitisha wagombea ili
kuwepo na uchaguzi wa haki.
Ameongeza fomu zitolewe kwa wogombea
wote na pale ambapo kiongozi yoyote ndani ya chama anawania nafasi ni
marufuku kuhusika kwenye mchakato wa uchaguzi, wabaki kuwa wagombea kama
wanachama wengine ili haki itendeke, na hii ni kwa nchi nzima.
"Kama
Katibu wa ngazi husika anagombea kamati ya siasa ichague mjumbe mmoja
miongoni mwa wajumbe asimamie uchaguzi, na kama Kamati nzima ya siasa
inagombea, ngazi ya juu iteue kiongozi mmoja asimamie uchaguzi huo ili
kujiepusha na ujanja ujanja wa baadhi ya viongozi wagombea kuficha fomu
kwa baadhi ya wagombea wenzao kwa maslahi yao binafsi badala ya
chama,"amesema Chongolo.
Pamoja na kupiga marufuku hiyo ,
Chongolo amepata nafasi ya kufafanua kwa kina namna ambavyo wanachama wa
Chama hicho kwa ngazi mbalimbali kuendelea kushirikiana na viongozi na
Wananchi kwa ujumla kufanikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo
inayotekelezwa na Serikali kwa niaba ya CCM.
Home
HABARI
KATIBU MKUU CCM APIGA MARUFUKU VIONGOZI WANAOGOMBEA KUSIMAMIA UCHAGUZI, ATAKA HAKI ITENDEKE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...