Na Mwandishi wetu, Michuzi Tv Pwani

Mamlaka ya Majisafi  na Usafi wa Mazingira Dar-es-salaam imepongezwa kwa kuweza kufanya mabadiliko ya fikra za wafanyakazi kiasi cha kuweza kuboresha huduma na tija katika Mamlaka hiyo.

Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Katanga alipotembelea mradi wa ujenzi wa Bandari Kavu ya Kwala ambapo DAWASA inatarajiwa kujenga mradi mkubwa wa maji wenye kuhusisha tenk kubwa la ujazo lita elfu 10. 

Akizungumza katika ziara ya ukaguzi wa miundombinu mbalimbali ambayo itakwenda pia kuhudumia eneo maalum la Viwanda la Kwala, Katibu Mkuu Kiongozi alisema serikali imedhamiria kuona watumishi wa umma wakifanya kazi kwa bidii na maarifa na kutaka taasisi nyingine za Umma kuiga mfano wa DAWASA.

Akizungumzia dhamira ya serikali katika kuvutia Wawekezaji na Mitaji, Balozi Katanga alisema nia ya serikali ni kuhakikisha kuwa mradi huo unakamilika kwa wakati huku ukiwa na miundombinu yote wezeshi na kwamba azma hiyi itafanikiwa endapo mipango iliyowekwa itatekelezwa kwa wakati na kwa ubora.

Kabla ya ziara hiyo, Balozi Katanga alipokea taarifa na maelezo ya miradi na mipango ya eneo hilo maalum la uwekezaji kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara za  Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Katibu Mkuu wa Wizara ya  Uwekezaji, Katibu Mkuu  Tamisemi, Katibu Mkuu Mawasiliano na Uchukuzi, Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara pamoja na Wakuu wa Taasisi zikiwemo DAWASA, Mamlaka ya Bandari, EPZA na Reli pamoja na Mwakilishi wa TANESCO.


Mapema Mtendaji Mkuu wa DAWASA Eng. Cyprian Luhemeja alieleza kuwa tayari DAWASA imefanya usanifu wa awali wa kupeleka maji katika eneo hilo ambapo lengo ni kujenga kituo cha kusukuma maji Vigwaza na bomba kuu la inchi 12 la kusafisha maji, tenki la ujazo wa lita milioni 10 na mabomba ya usambazaji maji. 


Lengo la mkutano na ziara hiyo ya Katibu Mkuu Kiongozi ni kukutanisha wadau wote ili kuweza kukamilisha kazi ya ujenzi wa bandari kavu na eneo maalum la biashara ambalo linatarajiwa kuwa moja ya vituo vikuu vya kibiashara Africa.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Katanga Akizungumza na Watumishi wa Tasisi mbalimbali alipotembelea mradi wa ujenzi wa Bandari Kavu ya Kwala ambapo DAWASA inatarajiwa kujenga mradi mkubwa wa maji wenye kuhusisha tenk kubwa la ujazo lita elfu 10. 
Mtendaji Mkuu wa DAWASA Eng. Cyprian Luhemeja Akieleza utayari wa Dawasa wa kusambaza katika bandari kavu ya Kwala mkoani Pwani
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Katanga Akizungumza na Watumishi mbalimbali akiwemo Mtendaji Mkuu DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Katanga Akiwa amemshika mkono Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Katanga Akizungumza na Watumishi kutoka tasisi mbalimbali 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...