Na Mwandishi wetu Mirerani
KATIBU
Mtendaji wa Tume ya Madini nchini mhandisi Yahaya Samamba anatarajia
kufanya ziara Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara,
jumatatu ya Mei 16 mwaka huu.
Afisa
madini mkazi (RMO) wa mkoa wa kimadini wa Simanjiro, Fabian Mshai
amesema Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini atakutana na wamiliki wa
migodi, mameneja na wataalamu wa kulipua miamba ya migodi.
RMO
Mshai amesema pamoja na kuzungumza na wadau hao wa madini pia
atasikiliza changamoto mbalimbali zinazowakabili wachimbaji madini.
Amesema
kiongozi huyo akiwa na wasaidizi wake pia atawajazia uwezo zaidi kwa
kutoa elimu ya uchimbaji na ufanyaji kazi salama ili kuepusha ajali
migodini.
"Wamiliki wote
wa migodi, mameneja na walipuzi wa migodi ya madini wa Mirerani,
Mwajanga, Landanai, Nadonjuki, Kitwai na maeneo mengine wanakaribishwa
kwenye kikao hicho.
Katibu
wa chama cha wachimbaji madini Mkoa wa Manyara, Tariq Kibwe amewaasa
wadau hao wa madini kujitokeza kwa wingi ili kukutana na kiongozi huyo
ambaye pia atasikiliza kero za wachimbaji.
"Changamoto
mbalimbali za kuhusu uchimbaji ambazo haziwezi kutatuliwa kwenye ngazi
ya RMO zinapaswa kufikishwa kwake hivyo wajitokeze kwa wingi," amesema
Kibwe.
Mmoja kati ya
mameneja wa migodi ya madini ya Tanzanite, Rashid Mohamed amesema hiyo
ni fursa nzuri kwao kukutana na kiongozi huyo mkubwa kwenye sekta ya
madini.
"Tutashiriki kwa
wingi kwenye kikao hicho kwa lengo la kujaziwa uwezo zaidi kwani RMO
amesema tutapatiwa elimu juu ya masuala ya uchimbaji madini," amesema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...