Na Amiri Kilagalila,Njombe

Mkuu wa mkoa wa Njombe Waziri Kindamba ameagiza watoa huduma za afya katika mkoa huo kuboresha zaidi mahusiano baina yao na wateja katika sehemu zao za kutoa huduma za afya, ili kuongeza kiwango cha mteja kuridhika na huduma wanazozipata katika kuimarisha afya zao.

Ametoa agizo hilo wakati akizindua kituo cha afya Marie Stopes Makambako Polyclinic kilichopo kata ya Kitisi katika halmashauri ya mji wa Makambako mkoani humo.

Aidha Kindamba ametoa wito kwa waganga wakuu wa halmashauri na wilaya za mkoa huo kushirikiana na watoa huduma za afya kwenye vituo binafsi ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora.

“Nitumie pia fursa hii pia kuwasihi watoa huduma katika eneo la afya kuongeza ufanisi na upatikanaji wa huduma bora za afya katika maeneo mbali mbali ya mkoa huu ikiwa lengo kubwa ni kuhakikisha kila mtanzania anafikiwa na huduma naafuu na rafiki”alisema Kindamba

“Nitoe wito kwa mamlaka za serikali kupitia waganga wakuu wa wilaya kuendelea kutoa ushirikiano na kuboresha huduma za afya kwa wadau mbali mbali waliopo katika mkoa wetu kama tunavyoendelea kufanya katika kituo hiki cha Marie Stopes”aliongeza Kindamba

Mganga mkuu wa mkoa wa Njombe Dkt. Zabron Masatu amesema uzinduzi wa kituo hicho cha afya unafanya mkoa wa Njombe kuwa na jumla ya vituo 296 ambavyo vinatoa huduma ya mama na mtoto na kueleza kuwa vituo hivyo vitasaidia kupunguza changamoto ya vifo kwa akina mama na watoto.

“Kituo hiki cha Makambako ni kituo ambacho kitakuwa kinatoa huduma za kibingwa kwasababu kituo hiki kina daktari bingwa wa magonjwa ya akina mama na watoto,na sisi kama mkoa niahidi kumtumia huyu daktari kwenye maeneo zaidi ya hapa kwasababu halmashauri zote hazina daktari bingwa

Mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa na Mbunge wa jimbo la Makambako Deo Sanga wamesema kituo cha Marie stopes kitakua na msaada mkubwa kwa wananchi wa Makambako na maeneo mengine huku wakisisitiza kituo hicho kuwa na gharama rafiki za matibabu kwa wananchi.

Naye Mkuu wa shirika la maendeleo kutoka ubalozi wa Canada ambalo limefadhili ujenzi wa kituo cha afya cha Marie stopes Makambako Bi,Hellen Fytche amesema wataendelea kushirikiana na serikali katika kufikia malengo endelevu yanayohusu afya ikiwemo kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.

“Canada inachangia katika juhudi za serikali ya Tanzania katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu yanayohusiana na afya ikiwemo kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi,kuongezeka ufikiaji wa huduma ya elimu ya jinsia,kuboresha lishe kwa vijana na kuimarisha mfumo wa afya”alisema Bi, Hellen Fytche

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mkurugenzi mkuu wa shirika la Marie Stopes Tanzania Mr.Vadacanthara Chadrashekar amesema kituo hicho kimejengwa kwa ufadhili wa shirika la misaada la Canada kupitia ubalozi wa Canada nchini kikilenga kuhudumia wakazi wa mji wa Makambako na maeneo ya jirani ambao kwa sasa una wakazi wanaokadiriwa kufikia 116,398 ambapo asilimia 52% ni wanawake huku zaidi ya wananchi 850 wakiwa tayari wameanza kunufaika na kituo hicho cha afya.

Katika kuunga mkono juhudi za serikali Marie Stopes Tanzania ina zahanati na hospitali 9,moja iliyopo Zanzibar na nyingine zikiwa Tanzania bara.

Mkuu wa mkoa wa Njombe Waziri Kindamba akizungumza na wananchi wa Makambako waliojitokeza katika uzinduzi wa kituo cha afya mara baada ya kuzindua kituo cha afya.
Mkuu wa mkoa wa Njombe akikata utepe kuonyesha uzinduzi wa kituo cha Afya Marie Stopes kilichopo kata ya Kitisi mjini Makambako.

Mmoja wa watumishi wa kituo cha Afya  Marie Stopes akiendelea na shughuli ndani ya ofisi yake.

 
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Njombe mara baada ya uzinduzi wa kituo cha afya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...