Wakazi wa eneo la Goha kata ya Mkumbara wilayani Korogwe ambao wamekumbwa na adha ya uvamizi wa tembo kutoka mbuga ya Mkomazi wameiomba serikali kuiondolea kadhia hiyo kwa kujenga uzio katika eneo ambalo linatumiwa na tembo hao kuingia kwenye kijiji hicho.

Wakazi hao ambao wamejawa na hofu ya tembo ambao amao wameendelea kuonekana kila inapofika jioni wametoa rai hiyo mbele ya Mbunge wa Jimbo hilo, Timotheo Mnzava alipotembelea eneo hilo kuwafariji wakazi wa eneo ambao wegi wamepoteza mazao yao kutokana na uvamizi wa tembo.

Akizungumza katika kikao kilichofanyuka kijijini hapo, mkazi wa eneo hilo, Alhaji Abdallah Ramadhani Mangare alisema kuwa eneo hilo limekuwa likivamia wan tembo kuanzia miaka mingi iliyopita lakini imefika mahali ambapo serikali lazima ichukue hatua za kukomesha hali hiyo ili wananchi waishi kwa amani wakilima mazao ya na kufanya shughuli nyingine za kiuchumi.

Alisema tembo hawa wala si mara ya kwanza kuja. “Kila mwaka wanakuja hususan mwezi wa saba. Hatuwezi kuwaua. Kama zamani ambapo walikuwa wanakuja mabwana nyama na kupiga wawili watatu halafu wanatokomea. Tembo ni wetu na tena ni wa kimataifa hivyo suluhisho ni uZio,” alisema.

Alihaji Mangare alisema kuwa uzio umeonyesha uwezo wa kuwazuia kama ilivyo kwa mwekezaji mmoja aitwaye Mjordani ambaye ameweza kuzuia tembo kwa uzio.

Pia alitoa rai ya serikali kujenga bwawa kwenye eneo wanaloingilia ambalo litawafanya wasiendelee kuja wakikuta maji.

“Uvumilivu una mwisho. Nimeacha kulima vitunguu, nyanya na kabichi kwa sababu tembo wamenikataza,” aliwachekesha watu waliohudhuria kikao hicho.

Aidha aliwataka maafisa wanyama pori kutoka Mbuga ya Taifa ya mkomazi waliokuja hapo kwa ajili ya kuwaswaga tembio hao warejee katika mbuga kuweka kambi katika eneo hilo badala ya kuweka mbali na eneo hilo.

Mwingine, Idi Uledi aliwataka maafisa wa wanyamapori kutumia utaalamu wapo kuwahamisha tembo hao ili wakazi wa eneo hilo wasiwe ombaomba kwa kukosa mazao yanayowaletea kipato.

Nao wakina mama walielezea hofu yao ya wanaume kuanza kukimbia eneo hilo kutafuta shughuli za kipato katika eneo jingine wakiwaacha wake zao na watoto wakiteseka kwenye kijiji hicho.

Pili Stella Kombo alisema kuwa tembo hao wamechafua mashamba ya mpunga na hata kama watalipwa fidia haiwezi kufanana na kipato wanachopata kutokana na kilimo hicho.

“Hapa tulipo tembo wanakuja. Tunaogopa hata wanaume wanaweza kukimbia eneo hili.

Naye Zaina Bakari Sabuni alisema kuwa ukiangalia tembo walichifanya kwenye mashamba ya mpunga mtu anaweza akalia. “Ndoa zetu ziko mashakani. Kuna hatari kina baba wataondoka katika eneo hili. Tunamwomba Mama Samia atusaidie. Kuna ndoa zimeanza kukatika,” alisema Sabuni

Naye Salima Abedi alieleza hofu yake juu ya watoto wadogo wanaokwenda shule ambayo iko karibu kabisa na mashamba yanayovurugwa na tembo.

Mkuu wa Wahifadhi watatu walioletwa kwa ajili ya kazi hiyo, Baraka Zedekia alisema kuwa kuna tembo nane (8) ambao ndio wanaosumbua na aliahidi kuwa watafanya juhudi kuwarejesha katika mbuga.

Ofisa huyo ambaye ailazimika kuondoka kabla ya kikao kumalizika baada ya kuletewa taarifa ya kuonekana kwa tembo hao aliwataka wananchi kuwa watulivu na kutoa ushirikiano ili wawaondoe tembo hao.

Mbunge wa jimbo hilo ambaye alitembelea shamba la Mkonge na mashamba ya mpunga yaliyovurugwa na tembo alisema historia ya uvamizi wa tembo inaonyesha kuwa mabli na mazao yanayoharibika jumla ya watu watatu wamethibiishwa kuuawa na tembo kuanzia mwaka 2009 hadi mwaka huu.

Mnzava alieleza kuwa serikali imechukua hatua ya kuleta maafusa kutoka Mamlaka ya Wanyamapori (TAWA) na kuwataka wananchi washirikiane nao kuondoa kadhia hiyo.

Pia alisema kuwa wamkubalina na Wizara ya Maliasili kuwa wamaafisa hao hawataondoka hadi tembo hao wawe wameondoka katika eneo hilo.

Akizungumzia hasara waliyopata wananchi alisema kuwa serikali itafanya tathmini kwa wakulima waliopata madhila hayo kwa nia ya kuwalipa fidia ingawa alikri kuwa kiasi kinacholipwa si kikubwa kulipia hasara anayopata mwananchi.

Alisema kuwa kiwango kinacholipwa ni cha miaka ya 1990 na sasa hivi wao kama wawakilishi wa wananchi wameanza kuipigia kelele serikali ili ilipe kiwango ambacho angalau kinafanana na hasara wanayopata wananchi wanaoharibiwa amazao yao na wanyamapori.

“serikali inasema ni mzigo lakini na sisi maumivu tunayopata ni makubwa,” alisema na kuahidi kuwa atahakikisha malipo yanafanyika mapema. “Safari hii tunachukua hatua haraka na hatusubiri mtu afe,” alisema.

Mnzava aliitaka TAWA kufanya kinachowezekana kuondoa adha hiyo akisisitiza kuwa wasipofanya hivyo wananchi watashindwa kuvumilia.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...