Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
Wekundu wa Simba SC wameondoka kifua mbele katika mchezo wao wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar baada ya kuondoka na ushindi wa bao 2-0 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Mabao ya Simba SC kwenye mchezo huo yamefungwa na Mshambuliaji Kibu Dennis dakika ya 13 akifunga bao la kwanza na bao la likifungwa na Mshambuliaji John Bocco dakika ya 29, huku wakitawala mchezo kwa muda mrefu.
Kwa matokeo hayo, Simba SC wanafikisha alama 49 wakiwa nyuma ya vinara Yanga SC wenye alama 57, wote wakiwa na michezo 23. Simba SC imepunguza ‘gap’ na sasa watakuwa wamebakisha alama 8 kuwafikia Watani wao wa Jadi Yanga SC.
Kagera Sugar wamefikisha alama 29 wakiwa kwenye nafasi ya 7 ya Msimamo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara msimu huu.
Hata hivyo, Ligi hiyo iliendelea kwa michezo mbalimbali ambapo, Polisi Tanzania FC walipata sare ya 0-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC katika dimba la Ushirika mjini Moshi, huku Coastal Union FC wakipata ushindi wa bao 1-0 mbele ya Biashara United Mara katika uwanja wa CCM Mkwakwani, Tanga.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...