Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan Mitawi amesema changamoto ya kukatika kwa mawasiliano inayowakabili wananchi wa Kijiji cha Swipese, Pemba inatarajiwa kumalizwa na ujenzi wa kivuko cha watembea kwa miguu katika eneo hilo.

Tathmini ilionesha kuwa maji ya bahari yameingia katika maeneo ya kilimo cha mpunga na wananchi wa Shehia ya Mkungu kijijini hapo hivyo kujaa kwa maji haya pia kumesababisha kukatika kwa mawasiliano kutoka upande wa pili takribani kilometa 3.3.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya mradi huo kwa Mkandarasi Dezo Civil Contractors Co. Limited kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi, Mary Maganga katika eneo la Kwa Mgogo wilayani Mkoani, Mkoa wa Kaskazini, Mitawi alisema ujenzi huo utagharimu sh. bilioni 1.2.

Alisema kivuko hicho katachojengwa kwa kiwango cha juu na kudumu kwa miaka takriban 40 bila kufanyiwa ukarabati, litakuwa msaada mkubwa kwa wananchi hao kwa kuwapunguzia adha ya kuvuka inayowakabili ambapo ujenzi wake utakuwa wa kipindi cha miezi 18.

Mitawi alisema utekelezaji wa mradi huo ni matunda ya ziara za viongozi mbalimbali wa kitaifa walizofanya kwa nyakati tofauti tangu mwaka 2019 na hivyo kuwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa mkandarasi huyo ili kazi ifanyike kwa haraka na ufanisi.

“Leo tumekuja kukabidhi eneo hili kwa mkandarasi kwa ajili ya kuanza ujenzi mara moja na tunatarajia atakamilisha chini ya muda uliopanga kama alivyofanya katika maeneo mengine, niwaombe wananchi mtoe ushirikiano kwa mkandarasi atakapohitaji eneo la kuweka vifaa vya ujenzi na pia kwa mujibu wa maelekezo ya Mheshimiwa Makamu wa Pili kuwa kwa zile shughuli ndogondogo kipaumbele kiwe kwa wakazi wa hapa,” alisema Mitawi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzubar Bw. Thabit Idarous Faina alisema kuwa athari hizi za kimazingira zimewakabili wananchi wa eneo hilo kwa kipindi cha muda mrefu kiasi cha kusababisha washindwe kuvuka upande mmoja kwenda mwingine kufuata mahitaji ya kila siku.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Kusini Mattar Zahor Masoud akizungumza ofisini kwake wakati viongozi hao walipofika kujitambulisha, aliahidi kutoa ushirikiano kwa mkandarasi na kusema kukamilika kwa mradi huo kutasaidia shughuli kulihifadhi eneo hilo sambamba na kufanya shughuli za uchumi kufanyika kwa urahisi.

Pia mkuu wa mkoa huyo alisema kuwa atashiriki katika usimamizi mzima wa mradi huo kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ili uweze kukamilika kwa wakati na kwa ufanisi mkubwa  

Eneo lina changamoto kubwa kupata mrai ni faraja kubwa itasaidia shughi za kiucbumi na hfadhi ahidi kutoa ushirikianao wanadarasi watakapokuwa na shuhujuli za ujenzi miradi yte katika mkoa wasiiamia wakuu marc na madc

Faina alibainisha kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) imeshirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibara (SMZ) kupitia Afisi yake na Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais imechukua juhudi za kuhakisha wananchi wanatatuliwa changamoto hiyo.

Nao wanachi wa eneo la Kwa Mgogo katika Kijiji cha Sipwese walionesha furaha yao kutokana na ujio wa mradi huo na kuzishukuru Serikali za pande zote mbili kwa ushirikiano na kutekeleza mradi huo wakisema utaleta manufaa makubwa kwao.

Simai Juma Silima alisema wakazi hao wamekuwa wakipata adha kubwa kushindwa kufanya kilimo kwasababu eneo hilo limekuwa na maji chumvi, kukosa maji safi na salama na kushindwa kuvuka kutoka upande mmoja kwenda mwingine.

Nae Bi. Fatma Simai Haji alisema kuwa watoto wao wamekuwa wakivuka kwa tabu na wakati mwingine wakishindwa kwenda skuli na hivyo kushindwa kuhudhuria masomo, hivyo kivuko hicho kitakuwa msaada mkubwa kwao.

“Tangu wazee wetu na leo hii tumekuwa tukipata adha kubwa katika kuvuka tunashindwa kwenda shamba wala madukani, watoto wetu wanakwenda shule madaftari yanalowa tunashukuru kwa mradi huu sasa tatizo hili litaisha,” alisema

Itakumbukwa mkataba wa ujenzi huo ulisainiwa kati ya Katibu Mkuu Bi. Mary Maganga na Bw. Premji Pindoria kwa upande Dezo Civil Contractors Co. Limited katika Ofisi ya Makamu wa Rais Mtumba jijini Dodoma Machi 31, 2022.

Aidha, makabidhiano ya eneo la mradi kwa SMZ yalifanyika Machi 30, 2022 na kushuhudiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.

Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan Mitawi (wa pili kushoto mwenye kofia) akizungumza wakati wa makabidhiano ya mradi wa ujenzi wa kivuko cha waenda kwa miguu kwa kwa Mkandarasi Dezo Civil Contractors Co. Limited katika eneo la Kwa Mgogo Kijiji cha Sipwese Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kaskazini Pemba. Wengine wa tatu kushoto ni Katibu Mkuu Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Thabit Idarous Faina na kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Bi. Farhat Ali Mbarouk.

Mmoja wa wananchi wa la Kwa Mgogo Kijiji cha Sipwese Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kaskazini Pemba akivuka maji kutoka upande mmoja kwenda mwingine kutokana na athari za maji ya bahari kufurika katika eneo hilo, tayari Serikali imeanza hatua ya mradi wa ujenzi wa kivuko kitakachowasaidia kuvuka.

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Mattar Zahor Masoud akizungumza ofisini kwake na viongozi waliofika kujitmbulisha kabla ya kufika eneo la makabidhiano ya ujenzi wa mradi wa kivuko cha waenda kwa miguu Kijiji cha Sipwese Wilaya ya Mkoani.

Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan Mitawi na viongozi mbalimbali akiwa katika litakalojengwa la mradi wa ujenzi wa kivuko cha waenda kwa miguu Kijiji cha Swipese, Pemba.

(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)

 

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...