.- Ampongeza Msanii Alikiba kwa kuandaa bonanza la Usafi Tabata.

 Asema Filamu ya Royal tour iliyozinduliwa na Rais Samia Suluhu Hassan imekuja wakati muafaka ambapo mazingira ya Dar es salaam ni safi na yanavutia Watalii.

Na Humphrey Shao, Michuzi Tv

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla na balozi wa Mazingira kupita Kampeni ya Safisha Pendezesha Dar es salaam Msanii Ally Selehe Kiba almaarufu Kama Alikiba wamefanya Usafi wa pamoja eneo la Tabata ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa Mkoa kufanya Usafi kila Jumamos ya mwisho wa Mwezi.

Akizungumza wakati wa zoezi Hilo lililokwenda sambamba na bonanza, RC Makalla amepongeza Wakazi wa Dar es salaam kwa mwamko mkubwa wa kufanya Usafi jambo linalofanya Jiji Hilo kushika nafasi ya sita kwa Usafi Barani Africa.

Aidha RC Makalla amempongeza Msanii Alikiba kwa kuratibu vizuri zoezi la Usafi wa pamoja siku ya Leo kwa kushirikiana na vikundi mbalimbali.

Pamoja na hayo RC Makalla ametumia hafla hiyo kuwahimiza Wananchi kuheshimu Mambo matano yaliyokatazwa ikiwemo Ufanyaji biashara kwenye maeneo yaliyokatazwa, biashara kwenye njia ya watembea kwa miguu, hifadhi ya Barabara, Ufanyaji biashara juu ya Mitaro pamoja na Ufanyaji biashara mbele ya Taasisi za umma ikiwemo Shule.

Hata hivyo RC Makalla amepokea msaada wa Vifaa mbalimbali vya Usafi kutoka kwa Wadau walioguswa na jitiada za Mkoa katika kusafisha mazingira kupitia Kampeni ya Safisha Pendezesha Dar es salaam.

Kwa upande wake Msanii Alikiba ameahidi kuendelea kushirikiana na RC Makalla katika kuhakikisha Jiji la Dar es salaam linaendelea kuwa safi ambapo ametoa wito kwa Wananchi kufanya Usafi.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla akiongoza Zoezi la Usafi katika eneo la Tabata Mkoa Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akizoa taka wakati wa zoezi la Safisha pendezesha Dar es Salaam
Msanii Alli Kiba akifagia mtaro wa barabra katika eneo la Tabata Barakuda




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...