Na Amiri Kilagalila,Njombe

Kufuatia changamoto ya idadi kubwa ya wanafunzi na kupelekea kukaa kwa shida madarasani katika shule ya sekondari Kipagamo iliyopo kata ya Makambako wilayani Njombe imeisukuma benki ya biashara Tanzania (TCB) kutoa msaada wa viti na meza vyenye thamani ya zaidi ya Milioni 1.8 na kumaliza changamoto hiyo.

Akiweka bayana sababu za kuishika mkono shule hiyo meneja wa TCB tawi la Makambako David Mwakila amesema ni shida kubwa waliyokuwa wakipata wanafunzi na kwamba wameamua kusaidia serikali na wazazi kumaliza tatizo hilo ili kuboresha mazingira ya kutoa na kupokea elimu ili kuongeza ufaulu.

Awali mkuu wa shule hiyo ya sekondari Rahab Sandagila na afisa elimu Sekondari katika Halmashauri ya mji wa Makambako Aderick Nombo wanasema msaada huo unakwenda kumaliza changamoto ya viti meza huku pia wakiomba wadau wengine kuto sita kuwasaidia ujenzi wa ukumbi nanBweni ili watoto wawe muda wote shule.

Kwa upande wao wananfunzin akiwemo Joyce mgeni wanasema msaada huo umekuja muda muafaka na kwamba unakwenda kuleta matokeo chanya sio mrefu.

Tcb imetoka msaada wa viti 25 na meza 25 zenye Thamani ya Zaidi ya mil 1.8



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...