Na Humphrey Shao, Michuzi Tv

Leo tarehe 23 Mei 2022, Taasis ya Lukiza Autsm , Imekabidhi msaada wa shilingi Mlioni nne na laki moja katika kituo cha ufundi cha SALT, kilchopo Mbezi ,Makabe Mkoani , Dar es saaam. Msaada huo wenye lengo la, Kuelimisha jamii kuhusu   ujumuishwaji wa watu wenye changamoto ya Usonji katika shuguhuli zote za afya,
 

Akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi msaada huo Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Lukiza Autism Foundatuon Bi. Hilda Nkabe amesema kuwa msaada huo ni utekelezaji wa malengo ya Lukiza Autism Foundation ya kuwawezesha vijana wenye Usonji na Ulemavu

"Fedha hizi tulizowapatia zitawasaidia katika mradi wao mpya wa kilimo cha kisasa ambapo wanakwenda kuanzisha ufugaji wa Kuku,Samaki na kilimo cha mbogamboga ndani ya eneo lao ili waweze kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa mboga kwa vijana waliopo kituoni." Amesema Hilda.

kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kituo Bi, Rebeca Lebi.Msaada huo umetolewa kwa nia moja ya kuwasaidia kiuchumi kwani mradi huo utapunguza gharama za ununuzi wa mahitaji ya chakula hapo kituoni.

"pesa hizo zitatumika kuendeleza mradi wa klimo mahiri cha mjini (ntensive urban farming) ambapo utajumuisha ufugaji wa samaki kwa njia ya matanki, kilimo cha mbogamboga kwa matone na ufugaji wa kuku wa kienyeji.Pesa hizi zitasaidia mradi huu kuanza mara moja" Amesema Rebeca
 

Ametaja kuwa watoto wenye usonji mahitaji yao ya chakula ni Mbogamboga samaki na kuku hivyo wameona fedha hizo ziweze kusaidia mradi huo ili kuwajenga watoto na kuwa wenye afya bora.
 

Amesema wazazi wengi wamekuwa na tabia ya kuwaficha watoto wenye Usonji na ulemavu hivyo amewataka kutowaficha watoto wao na kuwapeleka katika vituo ambavyo vinasaidia kulea watoto hao ambao baadae wanakaa sawa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Lukiza Autism Foundation, Hilda Nkabe, akizungumza na Waandishi wa habari kabla ya kukabidhi hundi

Mkurugenzi Mtendaji wa kituo Bi, Rebeca Lebi.(Kulia) akitoa ufafanuzi kwa Waandishi wa habari

Mkurugenzi Mtendaji wa Lukiza Autism Foundation, Hilda Nkabe, (wa pili kushoto) akikabidhi mchango wa million 4.1 kwa kituo cha watoto wenye usonji kwa ajili ya vijana kuanza mradi wa kilimo na ufugaji. Kulia ni Mkurugenzi wa Kituo cha Salt Special, Rebeca Hudson, kulia ni Dkt wa Kituo Jordan Afrika, na kushoto ni Afisa Habari wa Lukiza Autism Foundation Frank Mshobozi, hafla iliyofanyika katika kituo cha SALT mbezi Makabe, jijini Dar es Salaam










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...