*Ahadi ya Madaraja kuongezewa limefanyika
.
*Wafanyakazi waongeza ufanisi wa kazi na kuleta matokeo kwa kuongezewa mshahara
Na Chalila Kibuda, Michuzi
Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania(TALGWU) kimesema kuwa Mei Mosi ya Mwaka huu imejibu kiu ya wafanyakazi juu ya kuongezwa mshahara kutokana na kukaa na miaka sita bila nyongeza hiyo.
Nyongeza mshahara huo ulitamkwa na Rais Samia Hassan Suluhu katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Mei Mosi iliyofanyika mkoani Dodoma.
Maadhimisho hayo yaliratibiwa TAlGWU Kitaifa ambapo Chama hicho maadhimisho ya kimempongeza rais Samia Suluhu Hassani kwa kuahidi kuongeza nyongeza ya mishahara kwa Wafanyakazi na kuamini kuwa Rais Samia hajawahi kuwaangusha wafanyakazi kwa kila alichokisema ametekeleza ikiwemo ile ya kupandishwa madaraja.
Akizungumza wakati wa kutoa tamko hilo Katibu Mkuu wa TALGWU Rashidi Mtima amesema kwamba ahadi alizozitoa rais Samia Suluhu Hassan katika maadhimisho hayo ikiwemo kuahidi kuongeza mishahara ya Wafanyakazi zimejenga ari ya kufanya kazi na kuleta matumaini mapya kwa Wafanyakazi ambayo yalikua yamepotea kwa miaka mingi.
"Tunamshukuru kwa kutuhakikishia nyongeza ya mishahara ambapo ni muda mrefu sasa Watumishi wa Umma hawajapandishiwa mishahara,hiki kilikua kilio chetu cha muda mrefu ambapo Sasa Jambo hili linaenda kutelekezwa kama alivyosema Mheshimiwa rais Samia Suluhu Hassani" amesisitiza Mtima.
Nakuongeza kuwa" tunatoa shukrani zetu za dhati kwa Mheshimiwa rais Samia kwa kuundwa kwa bodi yakupitia kima Cha chini cha Mishahara iliyopo sasa na kuagiza Wizara zinazohusika kuiwezesha bodi hiyo ili kutekeleza majukumu take ipasavyo.
Pia ameendelea kubainisha kwamba wamefurahishwa na kitendo Cha rais Samia kusikiliza kilio Cha muda mrefu kuhusu Watumishi walioondolewa kazini kwa vyeti vya kughushi (Feki) hivyo TALGWU Kama chama kwa kupitia Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini TUCTA wamekua wakiomba kwa muda mrefu serikali kuliangalia kundi hilo la Watanzania ambao walitumika kwa uadilifu,ambapo ameagiza Wizara ya Fedha na Mipango kushughulikia na kuwalipa stahiki zao zinazotokana na makato ya mishahara.
Katibu Mkuu huyo wa TALGWU kupitia tamko hilo amesema kwamba wanaishukiru serikali kwa kuagiza mifuko ya hifadhi ya jamii na maafisa Utumishi kuhakikisha wanashughulikia haki na stahiki za Watumishi wanaotarajiwa kustaafu ndani ya miezi sita ili pindi inapofika Mtumishi anastaafu mafao take yawe tayari hali ambayo inaondoa usumbufu kwa wanachama kwani wengi wao hutegemea mafao kwa ajili ya kuendeleza maisha yao.
Mtima amesema TALGWU imefurahishwa na kitendo cha serikali kuingilia Kati nakutoa maelekezo yakukemea kwa Wafanyabiashara wanaopandisha bei za bidhaa holela hali ambayo inapunguza uwezo wa Wafanyakazi kiweza kununua bidhaa na kukidhi mahitaji yake.
Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) Rashid Mtima akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na neema ya wafanyakazi kuongezwa mshahara kutokana na Kauli ya Rais Samia Hassan Suluhu wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi yaliyofanyika mkoani Dodoma
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...