Na Abdullatif Yunus - Michuzi TV

Shirika la Umeme Nchini Tanzania TANESCO Mkoa wa Kagera limeendelea na kuimarisha huduma pamoja na Miundo mbinu yake ili kuhakikisha huduma bora inapatikana wakati wote kwa Wananchi hususani wWateja wa Umeme.

Akiongea wakati wa Ukaguzi wa Ofisi ndogo ya kutolea Huduma za Dharula iliyopo Kemondo Halmashauri ya Wilaya Bukoba, Meneja wa Tanesco Mkoa wa Kagera Ndg. Godlove Mathayo amesema, Shirika linaendelea na kuboresha huduma zake kwa wateja na kwa kutambua hilo tayari Shirika limeanzisha Viunga (Ofisi ndogo) kumi na Tatu maeneo mbalimbali Mkoani Kagera ambavyo ni Ofisi ndogo, lengo likiwa ni kumsaidia Mteja kurahisishaupatikanaji wa Huduma ya Umeme ikiwa ni pamoja kutoa Taarifa na kushughulikiwa Tatizo lake kwa haraka, badala ya Mteja huyo kufunga Safari na kufuata huduma Makao Makuu ya Shirika jambo ambalo likiongeza usumbufu na gharama.

Meneja Godlove amesisitiza kuwa kwa Sasa Shirika lipo katika Mpango wa uboreshaji wa usambazaji Umeme kwa sehemu ya Wateja wanaopitiwa na laini kubwa ya Umeme kutoka kituo cha kupozea Umeme cha kibeta Manispaa ya Bukoba, hadi Muleba ikiwa ni awamu ya kwanza ya Utekelezaji, ambapo ujenzi wa laini hiyo kubwa tayari umekwishaanza na unatarajiwa kukamilika ifikapo Julai Mwaka huu, huku mzima kwa ujumla ukikadiriwa kugharimu fedha za Kitanzania shilingi Bilioni Nane.

Mpaka sasa Ofisi ndogo za kumi na Tatu (viunga) za TANESCO zimekwisha funguliwa maeneo mbalimbali Ikiwemo Izimbya, Izigo, Kyamorwa, Nshamba, Nyakanazi, Nyakahula, Rulenge, Benaco, Murongo, Nyakaiga, Nyaishozi, Rwambaizi na Mutukula.

 







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...