Na Mwandishi Wetu, Muleba

VIONGOZI wa Tanzania Peace Foundation wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Vijana Taifa Charles Sabiniani maarufu Lowasa wamewaomba Watanzania kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ameonesha uwezo mkubwa wa kuwatumikia katika kuleta maendeleo.

Wamesema hayo baada ya kutembelea Kituo cha Utalii kilichopo Kata ya Kamachumu wilayani Muleba mkoani Kagera. Kwenye kituo hicho kuna nyumba ya makumbusho ya Msonge iliyojaa kila aina ya historia ikiwemo ya kuwepo kwa zana za jadi zilizotumiwa na babu zetu wakati wa harakati za kupambana na Ukoloni.

Wakiwa katika nyumba hiyo wamejifunza mengi kuhusu historia ya Tanzania na Kabila la Wahaya na kwamba lengo la kutembelea kituo hicho ni kuonesha kwa vitendo kuunga mkono jitijada za Rais Samia aliyeamua kuitangaza nchi yetu kupitia filamu ya Royal Tour.

Akizungumza akiwa kwenye nyumba hiyo Sabiniani amesema Tanzania Peace Foundation wanatambua kazi kubwa na nzuri inayofanywa na Rais Samia katika kuutangaza utalii wa Tanzania, hivyo nao wanao wajibu wa kuunga mkono jitihada hizo.

“Binafsi sina shaka na uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan , pia sina shaka na uwezo wa Spika wa Bunge Dk.Tulia Ackson na uongozi mzima wa nchi.Kwa nafasi yangu nimekutana na vijana wengi katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu hakika wanajivunia uongozi mzuri wa Rais Samia, “amesema.

Ameongeza pamoja na mambo mengine yeye ni Mjasiriamali aliyefanya kazi na kampuni za nje, hivyo anajisikia fahari kuona marafiki zake walioko nje ya Tanzania hivi sasa wanataka kuja kuwekeza baada ya kuona filamu ya Royal Tour.

“Kupitia filamu ya Royal Tour tunayo nafasi ya kila mmoja wetu kumpongeza Rais Samia kwa uzalendo ambao ameuonesha kwa taifa letu na vijana wa nchi hii tutaendelea kumuombea maisha marefu na afya njema,”amesema Sabiniani.

Aidha amesema mbali ya kutembelea kituo hicho mwaka 2021 alipata nafasi ya kutembelea maeneo mengi ya kitalii likiwemo eneo la Kaole wilayani Bagamoyo ambapo alipata nafasi ya kuelezwa historia ya binti aliyekuwa na maajabu.

Amesema binti huyo aliyekuwa na uwezo mkubwa wa kutabiri inaelezwa mingi iliyopita aliwahi kueleza Taifa la Tanzania kuna mwaka litaongozwa na Rais mwanamke, utabiri ambao umetimia.

Ametoa mwito kwa Watanzania kuendelea kumuunga mkono Rais Samia pamoja na viongozi wengine waandamizi wa Serikali ya Awamu ya Sita huku akitumia nafasi hiyo kupongeza mafanikio yaliyopatikana ndani ya mwaka mmoja wa Rais.

Amesema Rais Samia ameendelea kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo kwa kasi jambo ambalo linaleta matumaini kwa walio wengi, hivyo kikubwa ni kuendelea kumuombea ili aendelee kulitumikia Taifa hili.

Katibu Mkuu Vijana Taifa wa Taasisi ya Tanzania Peace Foundation Charkes Sabiniani ( wa kwanza kushoto ) akiwa na viongozi wengine wa taasisi hiyo mkoa wa Kagera pamoja na viongozi wa CCM kata ya Kamachumu wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kutembelea kituo cha utalii kilichopo kwenye kata hiyo iliyopo wilayani Muleba mkoani Kagera.

 Viongozi wa Taasisi ya Tanzania Peace Foundation pamoja na viongozi wengine wa CCM Kata ya Kamachumu pamoja na baadhi ya wananchi wa eneo hilo wakiwa wameshika zana mbalimbali za jadi zilizopo katika kituo hicho

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...