Mkurugenzi wa Digitali na huduma za ziada kutoka Kampuni ya Vodacom, Nguvu Kamando amesema kampuni hiyo itahakikisha ubunifu unachangia katika maendeleo endelevu kupitia huduma wanazozitoa kwa jamii.

Amesema watahakikisha kuwa Tanzania ina kuwa miongoni mwa nchi zinazoendelea kidigitali kwa kufanya mageuzi katika sekta ya ubunifu ili kufikia uchumi unaotarajiwa.


Kamando ameyasema hayo leo Mei 12, jijjni Dar es Salaam katika wiki ya ubunifu ambayo kilele chake kinatarajiwa kuwa Dodoma Mei 19, mwaka huu
Amesema hii ni mara ya nne mfululizo kwa kampuni hiyo kuwa mdhamini mkuu wa Wiki ya Ubunifu Tanzania.


"Tunahakikisha hatumuachi mtu yoyote nyuma ya teknolojia kwani tunaendelea kuboresha huduma zaidi kwa ubunifu wa hali ya juu lengo ni kukidhi malengo na matakwa ya mtumiaji," amesema Kamando.

Ameongeza kuwa asilimia 60 ya watanzania ni vijana na kwamba ndio wanaotumia zaidi teknolojia, miundombinu na bidhaa za kidigitali katika kubuni vitu mbalimbali.

Kwa upande wake, Mwanzilishi wa Kituo cha Ubunifu cha hub 255, Jones Mrusha alisema kuwa tangu mwaka 2005, Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuimarisha sekta ya ubunifu.

Alisema hivi sasa kampuni changa zinaweza kuuza bunifu zao ndani na nje ya nchi hivyo, ni wakati wa kuwekeza katika mawazo bora yatakayotengeneza bunifu zenye tija kwa maendeleo ya watu.

"Serikali, sekta binafsi na vijana wenyewe wanatakiwa kushirikiana ili kuhakikisha sekta ya ubunifu inaleta manufaa kwa kuchangia pato la Taifa," alisema Mrusha.

Wiki ya Ubunifu inaratibiwa na Wizara ya Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na COSTECH na UNDP kupitia program yake ya Ubunifu-Funguo. Kilele cha wiki hiyo kinatarajiwa kufanyika kuanzia Mei 16 hadi 19, mwaka huu huko mkoani Dodoma.

Wadau katika ubunifu kutoka kulia, Rosemary Mwakitwange kutoka Taasisi ya East Africa Business, Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania PLC, Sitholizwe Mdlalose, Dkt Flora Tibazarwa kutoka UDSM Ecoteck na muwezeshaji Khalila Mbowe, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza majadiliano wakati wa  kongamano la wiki ya ubunifu (Innovation week 2022)  lenye mada ya ubunifu kwa maendeleo endelevu ambapo walizungumzia hali halisi ya ubunifu na teknolojia nchini na mategemeo yake kwa nyakati zijazo.
Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania PLC, Sitholizwe Mdlalose (katikati) akizungumza wakati wa  kongamano la wiki ya ubunifu (Innovation week 2022)  lenye mada ya ubunifu kwa maendeleo endelevu ambapo walizungumzia hali halisi ya ubunifu na teknolojia nchini na mategemeo yake kwa nyakati zijazo. Wengine kulia ni Rosemary Mwakitwange kutoka Taasisi ya East Africa Business and Media Training na Jonas Mrusha, muanzilishi wa Taasisi atamizi ya hub255.

Wadau wa ubunifu kutoka sehemu mbali mbali wakifurahia jambo kutoka kwa Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania PLC, Sitholizwe Mdlalose  wakati wa  kongamano la wiki ya ubunifu (Innovation week 2022)  lenye mada ya ubunifu kwa maendeleo endelevu ambapo walizungumzia hali halisi ya ubunifu na teknolojia nchini na mategemeo yake kwa nyakati zijazo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...