Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
Mkuu
wa mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge amewaasa wafanyabiashara na
wabebaji wa mkaa wanaotumia bodaboda , wavute subira wakati wakiendelea
kulipa tozo iliyopo kisheria ya sh.250 kwa kilo hadi hapo Waziri wa
maliasili na utalii atakapofanya mabadiliko kulingana na mapendekezo
yaliyotolewa.
Aidha ameeleza, viwango hivyo vya tozo vinatozwa kwa mujibu wa GN namba 59 ya January mosi mwaka 2020.
Akitolea
ufafanuzi wa malalamiko ya baadhi ya wafanyabiashara hao , kuhusiana na
madai ya tozo kubwa wanayolipa kwasasa kutoka 25,000 kwa gunia lenye
kilo 100 na kulipia kwa sh.37,500, Kunenge alisema mkoa umeshapokea
mapendekezo yote na watayafikisha kwa Waziri mwenye dhamana yafanyiwe
kazi.
"Viwango hivi vya
tozo vinatozwa kwa mujibu wa sheria ,Tunafahamu kumekuwepo mapendekezo
hayo ,jinsi ya kukusanya tozo hizo , mapendekezo mbalimbali yametufikia
na yapo ngazi ya mkoa Utaratibu unafanyika na yanashughulikiwa "
"Na
sisi tukiwa watendaji wa Serikali tumefahamu Lazima tufuate taratibu
ili tusiingie kwenye changamoto ya uvunjaji au ukiukwaji wa
sheria";alieleza Kunenge.
Alielezea
,anafahamu wananchi na wafanyabiashara Wana malalamiko Yao na Wajue
Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ni sikivu
itayafanyia kazi.
Kunenge
alibainisha ,Lengo la Serikali Ni kuongeza mapato na kuwasihi
wafanyabiashara hao wasikwepe ushuru kwani Ni chanzo Cha kushuka kwa
mapato.
Vilevile
mkuu huyo wa mkoa, alitoa Rai kwa wananchi kutumia Nishati mbadala na
wasitegemee Sana matumizi ya mkaa kwasababu Kuna kiwango Cha miti
ambacho hawawezi kuendelea kukata miti kwasababu ya athari ya tabia
nchi.
Baadhi
ya wafanyabiashara wa mkaa wanaofanya shughuli zao , Kibaha Vijijini
akiwemo Hosea Paulo na Yasin Rajabu ,wanaiomba Serikali mkoa na
wizara husika kuangalia kwa uchungu tozo waliyopandishiwa kutoka ushuru
wa 12,500 baadae TFS ikapandisha 25,000 na Sasa Bei ambayo inawaumiza
kulingana na maisha Ni 37,500 .
Nae Yasini alibainisha kwamba ,licha ya hayo bei ya shamba nayo ni kubwa 90,000 wakati zamani walilipia 60,000 .
Kwa
mujibu wa sheria ya misitu na.14 ya mwaka 2002 na kanuni zake
mfanyabiashara wa mkaa anatakiwa kulipa sh.250 kwa kila kilo ya mkaa au
12,500 kwa gunia lenye kilo 50.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...