Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetaka kasi utekelezaji wa maelekezo ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha korosho na mazao yote ya kibiashara mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara yanasafirishwa kupitia bandari ya Mtwara, tozo katika bandari hiyo zipitiwe na makasha/makontena yapatikane bandarini hapo yatekelezwe kwa kasi.
Hayo yamesemwa leo tarehe 05 Juni, 2022 na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndg Shaka Hamdu Shaka alipoitembelea Bandari ya Mtwara na kujionea ni kwa kiwango gani maelekezo hayo ya Mheshimiwa Rais yamefanyiwa kazi.
"Chama kinasisitiza kasi iongezeke katika kutekeleza Maelekezo ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu bandari ya Mtwara kutumika kusafirishia korosho na mazao yote ya kibiashara kwa mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara pamoja na hatua zingine za kuongeza ufanisi wa bandari hii kwani yana manufaa kwa Nchi na wananchi. Hivyo Chama kinaelekeza tena wizara ya Ujenzi na Uchukuzi maelekezo hayo yafanyiwe kazi kwa kasi zaidi." Amesema Shaka
Shaka amepongeza uamuzi wa serikali kuanza kusafirisha makaa ya mawe kwa kutumia bandari ya Mtwara kwani umeongeza tija kwa Mtwara na kwenye mapato ya serikali.
Ziara ya Shaka ya uimarishaji chama na ukaguzi wa utekelezaji wa ilani Mkoani Mtwara imemalizika leo.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM,
Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, akikagua baadhi ya maeneo
yanakopitia makaa ya mawe zikiwa ni hatua za kuyapokea, kuyahifadhi na
kuyasafirisha kwenda nchi mbalimbali.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM,
Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, akikagua Sheena ya pembejeo za
kilimo kwa ajili ya wakulima wa korosho mkoani Mtwara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...