Na MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

Dar es Salaam Mei 30, 2022: Jukwaa la CEO Roundtable of Tanzania (CEOrt) lilifanya hafla fupi ya kumuaga Mwenyekiti wake wa Bodi anayemaliza muda wake, Bw. Sanjay Rughani, kufuatia uhamisho wake nchi nyingine.

Bw. Rughani amefanya kazi na CEOrt kama Mwenyekiti wa Bodi tangu 2018, na kuwa mtu wa pili kushika nafasi hiyo tangu jukwaa hilo liliposajiliwa rasmi. Alichaguliwa na Bodi ya Wakurugenzi kumrithi Marehemu Mheshimiwa Ali Mufuruki. Na katika kipindi chote cha uongozi wake ameonyesha uongozi bora na kusaidia kuongoza shirika katika kipindi cha ukuaji mkubwa.

Wakati wa uongozi wake, Bw. Rughani alichukua jukumu muhimu katika kuzindua Programu ya CEO Apprenticeship Programme, mpango wa uongozi bora - juhudi za kitaifa za kujenga uwezo wa Wakurugenzi wakuu wenye maono kwa ajili ya siku zijazo. Pia alikuwa muhimu katika kuimarisha dhamira ya shirika katika uongozi wa kimaadili na kupambana na rushwa, ambapo 100% ya wanachama wa jukwaa sasa wametia saini Ahadi ya Taifa ya Uadilifu. Sambamba na dhamira ya CEOrt ya kutetea ajenda ya mabadiliko ya hali ya hewa, Bw. Rughani alikuwa mstari wa mbele kuhamasisha utekelezaji endelevu wa biashara, akiongoza kwa mfano na mara nyingi kuzungumza juu ya jukumu la sekta binafsi katika suala hilo. Aidha, wakati wa uenyekiti wake, CEOrt ilishuhudia ukuaji wa wanachama ukilinganisha na hapo awali ikiwa ni ongezeko la wanachama wapya zaidi ya 40%.

Akizungumzia mchango wa uongozi wa Bw. Rughani, Mkurugenzi Mtendaji wa CEOrt Bi. Santina Majengo Benson alieleza kuwa CEOrt imejawa na shukrani nyingi kufuatia mafanikio mengi katika kipindi cha uongozi wake. "Viongozi wa kipekee huleta mabadiliko, na tukiangalia kile Sanjay alichofanya hapa ni ushahidi tosha wa ubora wake," alisema. "Ametetea waziwazi miradi kadhaa yenye matokeo chanya ya kijamii na kiuchumi na tumeona matokeo. Kutoka katika kukuza uwakilishi wa wanawake katika uongozi hadi kuongoza juhudi zetu za ushirikiano na Serikali kwa madhumuni ya pamoja ya ustawi wa Tanzania, Sanjay anaacha alama ya kudumu katika shirika na nchini kote.”

CEOrt pia inachukua fursa hii kumkaribisha Bw. David Tarimo, Mshirika Mwandamizi Nchini wa PwC kama Mwenyekiti ajaye wa Bodi kuanzia tarehe 1 Juni 2022. Uzoefu wake ni pamoja na ushauri wa kodi na kufuata kodi kwa makampuni yanayofanya kazi nchini Tanzania na katika sekta mbalimbali, lakini kwa kuzingatia hasa madini, mafuta na gesi na huduma za muhimu. Pia anahusika sana katika mijadala ya kitaifa kuhusu masuala ya sera za kodi. Ndani ya PwC kanda ya Afrika David pia amewahi kuwa na majukumu ya uongozi wa kanda ya kodi.

Baada ya kujiunga na Bodi ya CEOrt mnamo Oktoba 2017, David ana nafasi nzuri ya kuliongoza jukwaa hilo katika kuendelea kuunga mkono matarajio ya serikali ya Tanzania kuleta mabadiliko kwa njia ya mazungumzo, na ushirikiano.

*********************************************



Mwenyekiti wa Bodi ya CEOrt anayemaliza muda wake, Sanjay Rughani (kulia) akiwa na Mwenyekiti anayepokea nafasi yake, David Tarimo (kushoto) katika hafla ya kumuaga Bw. Rughani tarehe 30 Mei 2022 Hyatt Regency, Dar es Salaam.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...