KATIKA kuhakikisha ukuaji wa sekta ya fedha nchini Mamlaka ya Masoko na Mitaji ya Dhamana (CMSA,) imekutana na wadau katika sekta ya masoko ya mitaji pamoja na Wizara ya Fedha na Mipango na kujadili utekelezaji wa mpango mkakati wa kuendeleza sekta ya fedha hususani katika masoko ya mitaji.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya
mkutano huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji ya
Dhamana (CMSA,) Nicodemus Mkama amesema mkutano huo umewakutanisha na
wadau mbalimbali zikiwemo benki na taasisi ambazo zimepata leseni kutoka
Mamlaka ya Masoko ya Mitaji, soko la hisa pamoja na soko la bidhaa na
wamekutana na kujadili mpango mkakati wa kuendeleza sekta ya fedha.
Amesema
katika mkutano huo wamejadili bidhaa mpya ambazo zitatolewa katika
masoko ya mitaji zitakazowesha sekta binafsi na Umma kupata fedha
zitakazotumika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta
hizo.
''Kampuni mbalimbali, Serikali zitaweza kutumia bidhaa
katika masoko ya mitaji kuweza kupata fedha zitakazotumika kutekeleza
miradi mbalimbali yenye tija kwa jamii.'' Amesema.
Mkama amesema
kuwa bidhaa hizo ni pamoja na kuuza hisa kwa kampuni na kutoa hati
fungani ambazo ni hati fungani za Serikali Kuu na hati fungani ambazo
zitatolewa na Halmashauri za mitaa na majiji, Manispaa na Miji ambapo
wataweza kupata fedha za kutekeleza miradi ambayo inaweza kujiendesha
kibiashara na kuweza kupunguza mzigo kwa Serikali Kuu.
Pia
amesema, utekelezaji wa mpango mkakati huo unategemewa kutekelezwa kwa
ufanisi kwa kipindi cha miaka mitatu ni pamoja na kutoa elimu kwa Umma
juu ya faida na fursa zinazopatikana katika masoko ya mitaji na kuna
mpango mkakati wa kuhakikisha watu wote mijini na vijijini wanaweza
kufikiwa.
''Katika kufanikisha hili kuna programu mbalimbali
ambazo zimewekwa katika mpango mkakati kwa kuhakikisha wananchi wote
wanafikiwa, na kuna mpango wa kuhakikisha vijana na makundi maalumu ya
wanawake na watu wenye walemavu wanafikiwa.... pia kuna programu maalum
zitakazofanyika katika vyuo vikuu na taasisi ya elimu ya juu kwa
kuhakikisha kwamba uelewa unajengwa katika makundi yote na wataalam
wakiwemo manesi, wanasheria, wahasibu wanafikiwa, tunaamini tutawafikia
asilimia 85 watanzania ndani ya miaka mitatu iyajo ili kujenga uelewa na
fursa zinazopatika katika masoko ya mitaji kwa wananchi wengi zaidi."
Amesema.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya FIMCO Ivan
Tarimo amesema mkutano huo ni fursa ya CMSA kwa kukaa na wadau wake
wakubwa na kujadili mpango mkakati katika kuyafikia malengo yao
kiufanisi kwa miaka mitatu iyajo.
Amesema ushiriki wa masoko ya
mitaji kwa watanzania bado ni mdogo licha ya kuwa na fursa lukuki
kiuchumi na kupata kipato, na kuwataka watanzania kuendelea kujifunza
kuhusu masoko ya mitaji.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...