Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Fatma
Nyangasa amemtaka mkandarasi Advent kufanya usambazaji wa miundombinu
ya maji mtaani kwa wakati ili wananchi kupata maji mara baada ya mradi
wa Kisarawe II kukamilika.
Ameyasema
hayo leo alipofanya ziara ya kukagua mradi wa maji wa Kisarawe II
pamoja na kuwasha pampu ya kisima kimoja kinachopeleka maji kwenye tanki
la maji lenye ujazo wa lita milioni 15 litakaloweza kutoa huduma ya
maji kwa wakazi wa Kigamboni na maeneo ya pembezoni.
"Namsisitiza
mkandarasi anayehusika na usambazaji wa miundombinu ambaye ni Advent
kuendana na muda walioutoa DAWASA wa miezi mitatu ili aendane kasi hiyo
na asilete sababu zozote kwani kila kitu kipo ili wananchi waanze kupata
Maji." Alisema Nyangasa
Nyangasa amewataka wananchi wa Kisarawe II pamoja na maeneo mengine ya Kigamboni
kuanza kufanya maombi ya kuunganishiwa maji ili mradi wa maji
unapokamilika waanze kutumia maji safi na salama na sio kusubilia mradi
umemalizika ndio wanaanza kuomba uunganishwaji wa maji.
Pia
amesema kisima kimoja kilichowashwa leo kinaweza kutoa huduma kwa nusu
siku kwa wakazi wa Kigamboni hivyo vikiwashwa visima vingine vitaweza
kumaliza changamoto ya upatikanaji wa maji katika wilaya ya Kigamboni.
"Kuna
utaratibu umeandaliwa na DAWASA ambapo mwananchi atakayetaka
kuunganishiwa maji atapewa gharama zake na kama atashindwa kulipia
gharama za kuunganishiwa maji basi ataunganishiwa kwa mkopo ili kuweza
kupata huduma ya maji huku akilipa kidogokidogo mkopo wake" alisema
Nyangasa
Naye
Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema mradi wa
Maji Kisarawe II unahusisha uendelezaji wa visima kumi na mbili vya maji
vyenye uwezo wa kuzalisha maji lita milioni 57 pamoja na ujenzi wa
tanki la kuhufadhia maji litakaloweza kuhifadhi maji lita Milioni 15
umefikia asilimia 95.
“Mradi
huu unatekelezwa kwa sehemu mbili, sehemu ya kwanza ni ujenzi wa kituo
cha kusukuma maji, kituo cha kupokea Maji, ulazaji wa mabomba ya maji na
ujenzi wa tanki kubwa la kuhifadhi maji la lita milioni kumi na tano
linalojengwa Kigamboni na awamu ya pili ikihusisha kazi ya kufunga njia
za umeme kwenye visima na kutoa maji kwenye visima na kupeleka kwenye
kituo cha kusukuma maji amesema Luhemeja.
Luhemeja
amesema Mradi huu ulianza kutekelezwa mwezi Disemba mwaka 2019 huku
ukigharimu kiasi cha bilioni 24 fedha za ndani za Mamlaka na kukamilika
kwakwe kutanufaisha wakazi 250,000 wa maeneo ya Kibada, Mjimwema,
Masonga, Kimbiji, Mpera na maeneo ya karibu.
Kwa
upande wa Diwani wa Kisarawe II Issa Hemed Zohoro ameiomba DAWASA kuipa
kiupaumbele kata ya Kisarawe II kwani ndio mzizi wa mradi huo wa Maji.
"Nitashangaa
Sana kuona wananchi wa kata ya Kisarawe II hawana maji lakini maeneo
mengine wamepata maji hivyo namuomba mkandarasi kuweza kukaa na DAWASA
ili kuangalia ni kwanamna gani tunaweza kupewa kiupaumbele" alisema
Zahiro
Mkuu
wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Fatma Nyangasa(kulia) akiwasha pampu ya
kisima cha kwanza kinachopeleka maji kwenye tanki la lita milioni 15
katika mradi wa maji Kisarawe II unaotekelezwa na DAWASA kushoto ni
Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja.
Mkuu
wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Fatma Nyangasa(kulia) akipata maelezo kutoka kwa
Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja(kushoto) kuhusu moja ya
kisima pamoja na pampu ya kusukumia maji wakati wa kuwasha pampu hiyo
katika mradi wa maji wa Kisarawe II unaotekelezwa na DAWASA.
Afisa
Mtendaji Mkuu DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akitolea ufafanuzi Tanki
la maji la Kisarawe II lenye ujazo wa Lita Milioni 15 linalojengwa na
DAWASA katika Wilaya ya Kigamboni Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara
ya Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Fatma Nyangasa ya kukagua mradi wa
maji wa Kisarawe II pamoja na kuwasha pampu ya kisima kimoja kati ya
Saba. Wa kwanza kushoto ni Diwani wa Kisarawe II Issa Hemed Zohoro
Mkuu
wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Fatma Nyangasa akizungumza wakati wa
kutembelea Mradi wa maji wa Kisarawe II ili kujiridhisha na kazi
inayofanywa na DAWASA ya kumaliza changamoto ya maji katika wilaya ya
Kigamboni
Mkuu
wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Fatma Nyangasa akiangalia maji yanayojazwa
kwenye Tanki la Kisarawe II lenye ujazo wa Lita Milioni 15 wakati wa
ziara yake ya kutembelea mradi huo.
Mkuu
wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Fatma Nyangasa akizungumza na waandishi wa
habari kuhusu namna Serikali iliyojipanga kumaliza changamoto ya maji
katika wilaya ya Kigamboni mara baada ya kumaliza ziara yake ya kukagua
ujenzi wa Tanki, uchimbaji wa visima kwenye mradi wa maji wa Kisarawe
II pamoja na kuwasha pampu ya kisima cha kwanza inayopeleka maji kwenye Tanki la lita milioni 15 .
Afisa
Mtendaji Mkuu DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza na waandishi
wa habari kuhusu DAWASA wanavyosimamia mradi wa maji wa Kisarawe II ili
uweze kumalizika kwa wakati na kuweza kuwaunganishia wananchi maji safi
na salama katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Kigamboni.
Diwani
wa Kisarawe II Issa Hemed Zohoro akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu Naman wananchi wa kata yake wanavyosubilia maji kwa hamu mara
baada ya mradi wa maji wa Kisarawe II kukamilika unaotekelezwa na DAWASA
katika Wilaya Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Msimamizi wa mradi kwa upande wa Advent, Mhandisi Michael Njau
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu zoezi la ulazaji wa mabomba
makubwa na madogo kwenye mradi wa maji wa Kisarawe II unaotekelezwa na
DAWASA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...