Na Khadija Seif, Michuzi TV
MSANII wa Singeli anaefanya vizuri kwa sasa anaetamba na vibao vingi vikali ikiwemo Haloo, Nakuja Balaa Mc aweka historia Kwa mara ya kwanza kwenye Muziki wa Singeli kwa kuachia albam yake "26 kipaji."

Balaa mapema leo Juni 17 ameiachia albam hiyo yenye jumla ya nyimbo 10 na zote akiimba mwenyewe bila kumshirikisha msanii yoyote yule.

hata hivyo ameeleza sababu ya kutoshirikisha msanii yoyote kwenye albam hiyo lengo likiwa ni kukuza kipaji chake na kuongeza thamani ya mziki wa Singeli.

"Naamini kupitia album hii ya Singeli na sisi wasanii tutapewa heshima kubwa na mziki wetu kuongezeka thamani zaidi."

Pia amewaomba mashabiki zake waweza kusikiliza album hiyo ya kwanza ya Singeli nchini na kuendelea kumpa ushirikiano wa kutosha.

Albam ya "26 kipaji" inapatikana wimbo wa chuki,bodaboda,Mama ashura,kasuku, bado naishi, najuta, msumbufu, nyingi, sichezi na wewe pamoja na mfano fupi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...