MAFINGA, IRINGA

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amefika na kukagua eneo ilipotokea ajali iliyosababisha vifo pamoja na majeruhi kadhaa ambao wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa wa Iringa.

Akiwa Mafinga mkoani Iringa IGP Sirro amewataka wamiliki wa magari yanayobeba abiria kuhakikisha wanakuwa na leseni inayowaruhusua kufanya biashara hiyo sambamba na kuwataka madereva wa vyombo vya moto kuzingatia kanuni na sheria za usalama barabarani kwa lengo la kuepusha ajali zinazoweza kujitokeza na kusababisha madhara ikiwemo vifo na majeruhi.

Katika hatua nyingine IGP Sirro amewatembelea majeruhi wanaopatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa wa Iringa na kuwapa pole kufuatia ajali waliyoipata.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...