IKIWA Juni 14 ya kila mwaka huadhimishwa siku ya wachangia damu dunia wafanyakazi wa Hoteli ya Johari Rotana ya jijini Dar es Salaam wamechangia damu katika hospitali ya Taifa Muhimbili ili kuhakikisha wanaokoa maisha ya watu.
Wamejitolea kuchangia damu ikiwa ni mara baada ya kupata taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa huduma za Kriniki katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Daktari Praxeda Ogweyo kuwa katika husipitali hiyo kunaupungufu wa damu.
Alisema kituo hicho kinahitaji uniti 120 hadi 150 za damu kwa siku lakini kinamudu kukusanya uniti 60 hadi 90 jambo ambalo huathiri shughuli katika Hospitali hiyo.

Mkurugenzi wa Chakula na Vinywaji wa Amos Chibaya na Afisa Rasilimali watu Aloyce Benza wa Hoteli ya Johari Rotana ya jijini Dar es Salaam wakichangia damu jijini Dar es Salaam leo Juni 15, 2022 katika hoteli hiyo kwaajili ya kusaidia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Mkurugenzi wa Utunzaji wa Nyumba wa Hoteli ya Johari Rotana, Suleiman Nyirenda (wa kwanza kushoto) na Mlinzi Hiyari Mohammed Mkari wakichangia damu jijini Dar es Salaam leo Juni 15, 2022, kwaajili ya kusaidia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili..jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...