Muonekano na Tuta kuu la bwawa la kufua umeme, Wajumbe wa Kamati ya Uwezeshaji ya Mradi wa kufua Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP), kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali (GFT) walifanya ziara ya kukagua eneo hilo June 6-8, 2022 mkoani Pwani.Muonekano wa eneo la kupeleka maji katika mitambo ya kufua umeme katika mradi wa JNHPP, Wajumbe wa Kamati ya Uwezeshaji ya Mradi wa kufua Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP), kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali (GFT)walifa nya ziara ya kukaua eneo hilo June 6-8, 2022 mkoani Pwani
Na Zuena Msuya, DSM
KAMATI ya Uwezeshaji ya Mradi wa kufua Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP), kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali (GFT) imeipongeza serikali kwa kupiga hatua zaidi katika utekelezaji wa ujenzi wa mradi huo.
Pongezi hizo zimetolewa na Meneja Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TAZARA) Mhandisi Fuad Abdallah kwa niaba ya wajumbe wote wa GFT wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi huo inayofanyika katika maeneo tofauti ya mradi huo, kuanzia June 6-11, mkoani Pwani.
Mhandisi Fuad alisema kuwa wamefanya ziara hiyo kwa kukagua maeneo mbalimbali ya mradi huo ambapo walikagua maendeleo ya ujenzi wa Tuta kuu la Bwawa, Kituo cha Kuchochea Umeme, Nyumba ya kuendeshea Mitambo ya kuzalisha umeme na Kingo za Bwawa (Saddle Dam)
Pia walikagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kudumu, barabara, Njia ya kupeleka maji kwenye mitambo ya kuzalisha umeme, Nyumba za Watumishi pamoja na eneo la Ufungaji wa Mitambo.
Sambamba na hilo walifanya ziara katika eneo litakalojengwa kituo cha kupoza umeme utakozalishwa katika mradi wa JNHPP na kuzambazwa katika maeneo mbalimbali nchini, kilichopo Chalinze mkoani Pwani, pamoja na njia ya kusafirisha umeme mkubwa wa Kilovolti 400 utakaozalishwa katika mradi huo.
“Huu ukaguzi tunaoufanya kila wakati, unatupa mwanga wa kile kinachoendelea katika mradi huu, sisi Kamati ya Uwezeshaji ya Mradi wa kufua Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP), tumeteuliwa kwa makusudi maalum ya kuhakikisha mradi huu unatekelezeka kwa wakati, kwa hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi huu tunaipongeza serikali”, alisema Mhandisi Fuad.
Kwa upande wake, mchumi mkuu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Yosepha Tamamu alisema kuwa ziara hiyo inatoa mwanya kwa wajumbe hao kuona na kueleza kwa uwazi na kufahamu matumizi sahihi ya fedha zinazotolewa na serikali katika kutekeleza mradi huo.
Tamamu alieleza kuwa pia inakuwa ni rahisi kwa wajumbe hao kueleza kwa kina na kwa uelewa mpana katika vikao vyao vya utekelezaji kwa kila taasisi husika ili kuona namna bora ya kuweza kukamilisha mradi huo kwa wakati na bila vikwazo vyovyote.
Kamati imekuwa ikifuatilia kwa karibu utekelezaji wa mradi huo tangu hatua za awali hadi sasa, ambapo pamoja na mambo mengine, baada ziara hiyo, imeridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa mradi huo na wanaimani kuwa utakamilika ndani ya muda uliopangwa.
Alieleza kuwa kamati hiyo imeundwa mahsusi ikihusisha wajumbe kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za serikali kwa lengo la kurahisisha na kufuatilia utekelezaji wa mradi kwa kuhakikisha majukumu yote katika makubaliano ya mkataba yanatekelezwa kwa wakati sahihi pamoja na kuishauri serikali.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambayo inaundwa na wajumbe 27, ambaye pia ni Mratibu wa mradi huo kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Christopher Bitesigirwe, alisema kuwa mpaka sasa serikali imeshalipa zaidi ya shilingi Trilioni 3.9 sawa na asilimia 60 ya malipo yote na ni mradi ambao malipo yake yanaendelea vizuri.
Kwa mujibu wa Mhandisi Bitesigirwe,utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa JNHPP kwa ujumla umefikia hatua nzuri, huku kazi za ujenzi zikiendelea kwa lengo la kuzalisha Megawati 2115 za umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Bonde la Mto Rufiji.
Baada ya wajumbe hao kutembelea na kukagua maeneo mbalimbali ya utekelezaji wa ujenzi wa mradi huo, walifanya kikao cha pamoja na wameishauri serikali kupitia wizara na taasisi husika kutilia mkazo suala la kuhamasisha wananchi juu ya utunzaji wa vyanzo vya maji ili kuwezesha upatikanaji wa maji ya kuzalisha katika mradi wa JNHPP.
Wajumbe wa Kamati ya Uwezeshaji ya Mradi wa kufua Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP), kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali (GFT) wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa ziara ya kukagua mradi huo, iliyofanyika June 6-8, 2022, Mkoani Pwani.Wajumbe wa Kamati ya Uwezeshaji ya Mradi wa kufua Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP), kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali (GFT) wakitoka ndani ya handaki la kupeleka maji katika mitambo ya kufua umeme wakati wa ziara ya kukagua mradi huo, iliyofanyika June 6-8, 2022, Mkoani Pwani.Wajumbe wa Kamati ya Uwezeshaji ya Mradi wa kufua Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP), kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali (GFT) wakionyeshwa mchoro wa ramani wa kituo cha kupokea na kusambaza umeme kitakachojengwa eneo la Chalinze wakati wa ziara ya kukagua mradi huo, iliyofanyika June 6-8, 2022, Mkoani Pwani.Wajumbe wa Kamati ya Uwezeshaji ya Mradi wa kufua Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP), kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali (GFT) wakitazama moja na msingi wa nguzo kubwa zinazosimikwa kwa ajili ya kusafirisha umeme mkubwa wa Kilovolti 400 kutoka mradi wa JNHPP hadi Chalinze wakati wa ziara ya kukagua mradi huo, iliyofanyika June 6-8, 2022, Mkoani Pwani.Kazi ya kusafisha Eneo litakalojengwa kituo kikubwa cha kupokea na kusambaza umeme katika eneo la Chalinze mkoani Pwani, Wajumbe wa Kamati ya Uwezeshaji ya Mradi wa kufua Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP), kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali (GFT)walifa nya ziara ya kukaua eneo hilo June 6-8, 2022.Wajumbe wa Kamati ya Uwezeshaji ya Mradi wa kufua Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP), kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali (GFT) wakiwa katika majadiliano baada ya kufaya ziara ya kukagua mradi huo, iliyofanyika June 6-8, 2022, Mkoani Pwani.Mwenyekiti wa Kamati ya uwezeshaji ya Mradi wa Julius Nyerere(JNHPP, kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali(GFT) ambaye pia ni Mratibu wa mradi huo kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Christopher Bitesigirwe akizungumza na wajumbe wa Kamati hiyo wakati mkutano, baada ya ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo iliyofanyika Juni 6-8, 2022, mkoani Pwani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...