Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Ndugu Juma Duni Haji ametoa rai kwa Kikosi Kazi cha Rais cha Kuratibu Maoni ya Wadau Kuhusu Demokrasia kuzingatia matakwa ya Wananchi na maoni ya wadau katika Ripoti yao.
Rai hiyo imetolewa akiwahutubia Wanachama wa ACT Wazalendo katika Majimbo ya Tunduru Kusini na Tunduru Kaskazini jana tarehe 19 Juni 2022.

"Nilipokutana naye, nilimpongeza Mh. Rais Samia Suluhu kwa kuundwa kwa Kikosi Kazi ambacho kinawajibika kwake moja kwa moja. ACT Wazalendo tumepeleka maoni yetu ya kina kuhusu Tume Huru ya Uchaguzi, Katiba Mpya na maeneo mengine. Tunatoa rai kwa Kikosi Kazi kuzingatia ipasavyo maoni yaliyotolewa na wadau na kutanguliza mbele matakwa ya wananchi katika kutekeleza majukumu yake na kuandika Ripoti yao"-alisema Ndugu Ado.
"Haipendezi kuwa kila Uchaguzi ukija tunauwana na kuumizana. Nimemweleza Mh. Rais tulikomeshe hili. Tunahitaji Tume Huru ya Uchaguzi ili chaguzi zijazo ziwe za haki, huru na zenye kuaminika"-alisisitiza Ndugu Duni.

Katika hatua nyingine, Babu Duni aliwaeleza Wanachama wa ACT Wazalendo wa Tunduru kuwa ACT Wazalendo itaendelea kuupinga mfumo wa stakabadhi ghalani kwenye ununuzi wa mazao ya korosho, mbaazi, ufuta n.k kwa sababu haujaweza kutatua changamoto za wakulima hasa kuhusu kulipwa bei nzuri za mazao kwa wakati.

Pia, Babu Duni alitoa nasaha kwa Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Ndugu Julius Mtatiro kuzingatia haki za raia anapotekeleza majukumu yake.
"Mtatiro ni kijana wetu. Tulimpokea na kumpa nafasi. Akiwa upinzani aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Haki za Binadamu. Naambiwa hivi sasa amebadilika na anafikia hatua ya kutaka kuwafunga Wanawake wanaodai haki yao baada ya kuondolewa kazini kwenye Kiwanda cha kubangua Korosho. Namuomba abadilike na ajali haki"-Alihitimisha Babu Duni.

Mwenyekiti wa Chama yupo kwenye ziara ya ujenzi wa Chama kwenye Mikoa ya Mkoa wa Kichama wa Selous, Mtwara na Lindi kuanzia tarehe 19 hadi 21 Juni 2022. Ameambatana na Katibu Mkuu Ado Shaibu na Mjumbe wa Kamati Kuu Isihaka Mchinjita.

Akiwa kwenye Majimbo ya Tunduru Kusini na Tunduru Kaskazini amekagua ujenzi wa Ofisi ya Kata ya Ligoma na kuzindua ujenzi wa Ofisi ya Kata ya Muhuwesi.

Janeth Rithe, Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma, ACT Wazalendo.
20 Mei 2022.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...