Kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Newala Mkoani Mtwara imekamata mifuko ya Salfa ya unga 1230 inayodaiwa kwisha Kwa muda wake wa matumizi ilibaini Salfa hiyo chapa makonde bechi ya III kuuzwa Kwa wananchi.
Kwa mujibu wa katibu tawala wa wilaya hiyo Daniel Zenda katika operesheni iliyoendeshwa wilayani humo hivi karibuni ni kupoke maelekezo ya Katibu wa Halmashuri Kuu ya CCM Ndugu Shaka Hamdu Shaka ya kuvita kaka vyombo vya dola kuchunguza na kubaini mfanyabisha na kampuni ambazo zinaujumu mpango wa ugawaji Pembejeo zinazotolewa bure na serikali ya awamu ya Sita Chini ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.
Amefafanua kuwa katika hatua ya awali wamebaini Salfa kuwa na mabonge ambayo yanaiondolea sifa ya kutumika kwenye mikorosho
Zenda amewataka wananchi kutoa taarifa Kwa vyombo vya usalama pindi watakapobaini uwapo wa Salfa hiyo wilayani Newala.
Amewataka wakulima wilayani humo kuondoa hofu ya kusambaa Kwa pembejeo hiyo isiyofaa Kwa matumizi ya mikorosho na kwamba serikali ipo macho muda wote.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...