Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
Mashirika
yasiyo ya kiserikali, Mkoani Pwani yamemshukuru Rais Samia Suluhu
Hassan Kwakupewa ushirikiano na mazingira mazuri ya kuweza kutekeleza
Miradi mbalimbali katika jamii.
Hayo
yalisemwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Direct Aid Dr.Adam Othman wakati
wakizindua mradi wa kituo Cha elimu Cha taasisi ya wasioona ya Waisalmu
ya (VIMDAT) katika Kijiji Cha Mwanambaya mkuranga mkoani Pwani
Aidha
sheikh wa Mkoa Pwani alhaji khamisi Mtupa alizikumbusha mamlaka
kuwatendea wema wenye Uhitaji nchi kupata tahfifu ya Mungu.
awali
akisoma Risala Mwl.Musa njechele ametaja Changamoto mbalimbali
zinazowakabili ikiwemo Uhitaji wa Miundombinu ya Barabara Umeme na Maji.
Mkuu
wa Mkoa wa Pwani ,Abubakar Kunenge ameziasa Taasisi hizo licha ya
kuwajengea miundombinu na kuwapa taaluma pia wawazeshe walemavu hao
waweze kujiingizia kipato na kujitegemea
Akitoa
shukrani Rais wa Taasisi ya wasioona ya Waisalmu (VIMDAT) amempongeza
Rais Samia Suluhu Hassan Kwa Uongozi wake uliotukuka unao wajali watu
walemavu pia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...