TFS Lugalo Golf Open 2022, RC Makala anatarajiwa kuwa mgeni rasmi

Na Khadija Seif, Michuzi Tv

KLABU ya Lugalo Gofu jijini Dar es Salaam ikishirikiana na Wakala wa Misitu nchini (TFS) wameahidi kutunza mazingira na kuhakikisha viwanja vya Gofu vinakuwa katika hali nzuri na Miti ya kutosha pamoja na kuongeza Watalii nchini kupitia upekee wa vivutio vilivyopo kwenye viwanja vya Gofu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati akitambulisha rasmi Shindano la ‘TFS Lugalo Golf Open 2022’, Mwenyekiti wa Klabu ya Lugalo Gofu, Brigedia Jenerali (Mstaafu) Michael Luwongo amesema shindano hilo limefungua fursa mbalimbali ikiwemo watu mbalimbali kwa namna TFS wanavohudumia jamii na kuwapa elimu jinsi ya kuhifadhi Misitu, kununua Asali bora na upandaji Miti Kwa ajili ya kuboresha mazingira yanayotuzunguka na viwanja vya michezo ikiwemo vya Gofu.

“Mashindano haya yalikuwa yafanyike mapema Juni 5 lakini kutokana na washiriki kupewa muda zaidi ya kujiandaa, hivyo imebidi sasa rasmi yafanyike Juni 18 ambapo kupitia Wakala wa Misitu nchini (TFS) wadau na watu mbalimbali wamefaidika na elimu iliyokua ikitolewa kabla ya kutangaza shindano hili”.

Hata hivyo, Luwongo ametoa pongezi mbalimbali kwa wadau ambao wanaonyesha ushirikiano mkubwa katika mashindano yanayofanyika katika mchezo wa Gofu na kuhakikisha wanadhamini huku akiwataja TFS kama Mdhamini Mkuu wa shindano hilo pamoja na Serengeti Breweries ambao mara kwa mara wanatoa udhamini katika baadhi ya mashindano kuhakikisha siku ya Fainali washiriki wanapata vinywaji.

Kwa upande wake, Mdhamini Mkuu wa shindano hilo, Afisa Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS), Anna Lauo ameeleza namna wamekuwa wadhamini kwa mara ya 3 kuhakikisha mchezo wa Gofu unapewa nafasi kwenye jamii na kuwapa motisha watu mbalimbali kucheza mchezo huo ambao mara nyingi unaonekana wachezaji wake ni matajiri.

Hata hivyo, Lauo akaongeza kuwa kupitia elimu waliyoitoa kwa wadau na watu mbalimbali ambao walikua wakitembelea viwanja vya klabu ya Gofu Lugalo watahakikisha wanafanya juhudi za dhati kutunza mazingira.

“Kupitia viwanja vya Gofu tutahakikisha tunatunza mazingira na kuhakikisha kunapandwa miti ya kutosha mfano mzuri kiwanja cha Lugalo Gofu jijini Dar es salaam kuna mazingira mazuri yaliyosheheni Misitu pamoja, Miti na Mabwawa yakiwemo ndani ya viwanja hivyo”, amesema Lauo

Pia ametoa rai kwa wadau wa Misitu pamoja na Utalii kwa ujumla bila kusahau Sekta ya michezo kuhakikisha wana muunga mkono Mama Samia.

"Tutashirikiana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia kuutangaza Utalii, tumeona ameanza na Royal Tour, sisi tunamalizia kuendelea kuvutia Watalii kuja nchini kwetu, kuwekeza katika viwanja vya Gofu hivyo nakaribisha wadau mbalimbali kujitokeza kucheza mchezo huo pamoja na kuwekeza katika kutengeneza mazingira katika viwanja vya gofu”, ameeleza Lauo

Nahodha wa Klabu ya Lugalo Gofu, Meja Japhet Masai ameongeza mashindano hayo yataweza kushirikisha wachezaji ambao wamesajiliwa na Vyama vyao na wanatambulika kwa wenye viwango vinavokubalika.

Pia ametaja Mgeni rasmi katika kufunga mashindano hayo anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makala huku akifafanua kuwa tayari wachezaji wameshajisajili kushiriki shindano hilo na kusisitiza kuanza mapema saa 1 asubuhi siku ya ufunguzi.

"Mashindano hayana pingamizi katika Kila kipengele wachezaji watapewa zawadi washindi wawili tu na bila kusahau washindi wa mikwaju ya jumla watapatiwa zawadi na kwa siku ya ufunguzi mchezo utaanza mapema saa 1 asubuhi ikifuatiwa na siku ya kufunga mashindano sanjari na tafrija fupi tukiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makala.

Mwenyekiti wa Klabu ya lugalo gofu Mstaafu brigedia jenerali Michael Luwongo pichani akiwa na Mdhamini  kutoka Serengeti breweries Faith Moshi ambae ni Miongoni mwa wadhamini wa Shindano la "Tfs Lugalo golf open 2022" ambapo shindano hilo linatarajiwa kuanza rasmi Juni 18 mwaka huu katika viwanja vya Klabu ya lugalo gofu Jijini Dar es salaam
 Afisa Mkuu wakala wa Misitu nchini (TFS) Anna Lauo akizungumza wakati wa kutambulisha rasmi Shindano laTfs Lugalo golf open 2022" ambapo amewasihi wadau mbalimbali kuwekeza katika viwanja vya gofu nchini na kuhakikisha wanatunza Mazingira na kupanda miti kwa wingi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...