Makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla ( kushoto,) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya MIF Bi. Fatma Mwassa (kulia,) mara baada ya makabidhiano ya vifaa kwa ajili ya kuendeleza na kukuza ufaulu wa wanafunzi, Kusini Unguja.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwanamke Initiative Foundation (MIF,) Bi. Fatma Mwassa akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa hivyo na kueleza kuwa wataendelea kushirikiana na Serikali katika kukuza sekta ya Elimu nchini ili kujenga taifa imara.



KATIKA kuunga mkono jitihada za Serikali katika kukuza sekta ya Elimu nchini, Taasisi ya Mwanamke Initiative Foundation (MIF,) imetoa vifaa vyenye shilingi milioni 116 zilizoelekezwa katika kukuza kiwango cha elimu kwa vijana Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.

Akizungumza mara baada ya kupokea vifaa hivyo, Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla amesema azma ya Serikali ni kuhakikisha kiwango cha elimu visiwani humo inazidi kuimarika hasa katika miundombinu ya kujifunzia pamoja na utoshelevu wa walimu.

Amesema, jitihada za Serikali katika kuboresha sekta hiyo zinatekelezwa katika maeneo yote visiwani humo na mchango wa MIF katika kuboresha sekta hiyo ni hatua nzuri katika kuhakikisha kila mtoto anapata elimu bora na yenye manufaa.

"Jitihada hizi za MIF zinadhihirisha umuhimu wa sekta ya Elimu. Nimeona wakishiriki shughuli hizi kwa kuwasaidia watoto wa kike, nawapongeza kwa hili na tunatambua jitihada zenu." Amesema.

Aidha amewataka vijana kutambua jitihada hizo na kusoma kwa bidii ili wawe tija jamii na taifa kwa ujumla.

Akizungumza wakati wa kukabidhi fedha hizo,  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya MIF Bi. Fatma Mwasa amesema kuwa wataendelea kuunga mkono jitihada za kuinua kiwango cha elimu visiwani humo na kwa kutoa vifaa vyenye kiasi hicho cha shilingi milioni 116 wanaamini zitatatua changamoto na kuboresha baadhi ya maeneo.




Matukio mbalimbali wakati wa hafla ya makabidhiano ya fedha zipatazo shilingi milioni 116 zilizotolewa na Taasisi ya Mwanamke Initiative Foundation (MIF,)kwa ajili ya kuendeleza na kukuza ufaulu wa wanafunzi Kusini Unguja visiwani Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...