Na John Walter-Babati
KIONGO wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2022 Sahili Geraruma amezindua mradi wa maji wa Madunga katika halmashauri ya wilaya ya Babati wenye thamani ya Tsh. Milioni 190,085,038.66.
Mradi huo ambao umekamilika kwa asilimia 100 unakwenda kuwanufaisha wananchi wapatao 3,009 wa kijiji cha Gidng'war.
Kiongozi huyo amezindua Mradi huo baada ya kukagua na kuridhika na maendeleo ya ujenzi wake ambao umejengwa kwa fedha za kutoka kwenye mfuko wa maji wa taifa na programme ya lipa kwa matokeo (P for R).
Aidha ameagiza uongozi wa Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilayani hapo kuhakikisha wanawaonganishia huduma hiyo wananchi wa maeneo hayo.
Kauli mbiu ya mwenge wa uhuru mwaka 2022 "Sensa ni msingi wa Mipango ya maendeleo,shiriki kuhesabiwa tuyafikie maendeleo endelevu ya taifa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...