Naibu Waziri wa Afya, Mhe.Dkt Godwin Mollel amewapongeza watanzania wanaoishi nje ya nchi kwa kujitolea katika sekta mbali mbali na kuwa serikali itaendelea kuwaunga mkono katika kuhakikisha malengo yao yanafikiwa bila bugudha zozote za kiutendaji.

Ameyasema hayo katika uzinduzi wa shirika lisilo la kiserikali lenye chimbuko la DIASPORA la CAREUSTZ kwa niaba ya Waziri wa mambo ya nje , ambapo alisema kuwa kitendo cha Watanzania hao kuamua kufanya moja ya mradi wake wa masuala ya afya nchini ni jambo la kujivunia na kuwa wanapaswa kuungwa mkono.


Shirika hilo la CAREUSTZ AMBALO limesajiliwa hapa nchini na katika jimbo la Kentucky nchini Marekani liliweza kufanya huduma za matibabu nchini kwa muda wa wiki mbili kupitia mradi wao unajumuisha watoa tiba wanaotoka nchini marekani walioungana na madikitari mbalimbali wanaojitolea wa hapa nchini kutoa huduma za kiafya kwa walengwa wenye mazingira magumu.


Katika kipindi hicho huduma zilitolewa katika hospitali za Kairuki ,Dar es salaam,Baobab Mapinga Bagamoyo, Mnazi Mmoja, Zanzibar, na hospitali ya wilaya ya Bagamoyo ambapo jumla ya wagonjwa 1,000 waliweza kuhudumiwa na timu ya watoa tiba ya CAREUSTZ.

Pia mbali na huduma hiyo ,timu ya wauguzi wa shirika hilo imeshafanikiwa kufanya huduma ya matibabu kwa watoto 67 katika kituo cha Watoto wahitaji cha Watoto Wetu Tanzania .

Kwa upande wake Kiongozi wa Shirika hilo Profesa William Mkanta, ambaye ni Rais na Mwenyekiti wa Bodi ya CAREUSTZ aliishukuru serikali kwa kutambua mchango wa CAREUSTZ katika maendeleo ya jamii nchini na kuongeza kuwa wataendelea kuchochea watanzania wengine wanaoishi nje ya nchini(DIASPORA)kuleta maendeleo nchini.

Ameshukuru kwa ushirikiano unaoneshwa na Serikali kupitia wizara za Afya na wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki umethibitisha dhamira ya wizara na ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Mama Samia Hassan katika kuthamini mchango wa diaspora hapa nchini.

Katika hatua nyingine , Mhe. Mollel aliweza kutoa vyeti ya utambuzi wa huduma kwa madaktari wa kujitolea pamoja na taasisi zote za afya zilizoshirikiana na CAREUSTZ katika wiki mbili za mradi wa huduma za afya hapa nchini.






 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...