NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi ametoa wito kwa watumishi wa umma nchini kuepuka usumbufu na gharama za kwenda Dodoma kushughulikiwa changamoto zao na badala yake wapige simu za huduma kwa wateja ili waweze kuhudumiwa wakiwa popote walipo.
Ndejembi ametoa wito huo wakati alipojiunga na timu ya huduma kwa wateja Ofisi ya Rais Utumishi kupokea simu za watumishi wa umma mbalimbali ambapo ametoa majibu ya changamoto na malalamiko yanayowakabili watumishi hao.
" Nimeungana na timu yetu ya huduma kwa wateja kusikiliza changamoto zinazowakabili na kuzipatia ufumbuzi. Niendelee kutoa wito kwa watumishi wetu nchini kuepuka usumbufu wa kufunga safari kuja Dodoma kushughulikia changamoto zao badala yake wapige simu na watoa huduma wetu watazijibu papo hapo.
Niwaagize kitengo chetu cha huduma kwa wateja kusikiliza simu zote za watumishi kuanzia wale wanaofuatilia barua zao za uhamisho, wanaoulizia malimbikizo yao ya mishahara na wote wanaoulizia masuala yote ya kiutumishi, lengo la Ofisi ya Rais Utumishi ni kuondoa usumbufu wa watumishi wetu kusafiri umbali mrefu kuja Dodoma," Amesema Ndejembi.
Ndejembi amesema watumishi wa umma wanaweza kupiga namba 0262160240 ili waweze kuhudumiwa na kupatiwa ufumbuzi wa changamoto zao zote za kiutumishi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...