Watumishi wa ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu waaswa kuendelea kufuata maadili ya utumishi Umma kwa kufanya kazi vizuri na kuwa wabunifu katika utendaji wa kazi, ili kuepuka kufanya kazi kwa mazoea.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Dkt. John Jingu wakati wa semina kwa wafanyakazi wa Ofisi hiyo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Tume ya Uchaguzi Mjini Dodoma katika Kuadhimisha wiki ya utumishi wa umma; yenye kauli mbiu “Nafasi ya Mapinduzi ya nne kwa viwanda katika Masuala mapya yanayojitokeza kuhusu utoaji wa huduma na urejeshwaji wakati na baada ya janga la corona.”

“Serikali kupitia Mhe. Rais Samia Suluhu Hassani imeshatimiza wajibu wake kwa kuhakikisha maslahi ya wafanyakazi; marupupu, vitendea kazi vinapatikana, jukumu letu ni kuwajibika ipasavyo ili kuhakikisha kwamba wananchi wanafurahia huduma wanayopatiwa na serikali alisema, Dkt Jingu”

Alifafanua vikao hivi ni muhimu vinapaswa kufanyika mara kwa mara ili kuweza kujua mipaka ya kiutendaji wa kazi iko wapi. Lazima tufanye kazi kama timu kwa kuzingatia maslahi mapana ya Taifa.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu akizungumza katika semina ya watumishi wa Ofisi hiyo Uliofanyika katika ukumbi wa Tume ya Uchaguzi katika kuadhimisha wiki ya Utumishi wa umma.
Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu wakisikiliza na kufuatilia kwa umakini Dr. Revocatus Baltazary Ofisi ya Mganga Mkuu Jiji la Dodoma (hayupo pichani) katika semina iliyofanyika katika ukumbi wa Tume ya Uchaguzi katika kuadhimisha wiki ya Utumishi wa umma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu pamoja na Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Dkt. Wilson Charles na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Bwn. Kaspar Mmuya wakifutilia kwa umakini semina ya wafanyakazi kwa watumishi wa wizara hiyo iliyofanyika ukumbi wa tume ya Uchaguzi Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...