KATIKA kuendelea kuitangaza Filamu ya Royal tour Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Hassan Suluhu atakuwa mgeni Rasmi siku ya Chakula chenye asili ya Mkoa wa Kagera (KAGERA DINNER PART) kitakacholiwa katika viwanja vya kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam Juni 24 na 25, 2022

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Juni 11, 2022 Maratibu Mkuu wa Kagera Dinner Part, Ennock Bujuli amesema kuwa chakula hicho kimeandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na kuhamasisha amani na uzalendo nchini (TANUA), wakishirikiana na Kibangu Ruge English Medium ya jijini Dar es Salaam kuanzia saa mbili asubuhi (2:00).

Amesema kuwa lengo la kuanda chakula chenye asili ya watu wa kagera ni kuwakutanisha wanakagera ili kwa pamoja kutumia elimu yao, vipaji na karama zao kujadili jinsi ya kutumia jiografia ya mkoa wa Kagera ili kukumbushana tamaduni zao.

Amesema wakikutana pia watakumbushana na kutafuta namna ambazo zitasaidia kuvitangaza vivutio vya mkoa huo ndani na nje ya nchi.

"Wanakagera tumeandaa ngoma za Asili toka Kagera, Simulizi za wazee, Mafundisho ya ndoa bora, maonesho ya shughuli zinafanyika Kagera, chakula na burudani za kila aina." Amesema Bujuli

Amesema TANUA inatafsiri filamu ya Royal Tour katika awamu nne ambazo ni safari ya watunzi, wabunifu, waandishi, wawekezaji, wasindikaji na watanzania wazalendo kutembelea hifadhi za Burigi- Chato, Ibanda, Bweranyange, Bunena.

Amesema katika kukuza utalii wa ndani na ubunifu, Katika Mkesha wa kuukaribisha Mwaka 2023 wataenda kukesha katika kijiji cha Kizimkazi -Unguja ambako alizaliwa Rais Samia.

"TANUA Intelectual Centre itaunganisha watanzania Jasiri ili kufungua kituo cha Kutangaza Utajiri wa Tanzania ndani na nje ya nchi ambayo itaambatana na kufungua migahawa, Vituo vya kufundishia lugha ya Kiswahili." Amesema Bujili

Kwa upande wake Katibu wa maandalizi wa Kagera Dinner part, Kokuhirwa Bagwerwa Matovu amesema kuwa Katika Chakula hicho chenye asili ya Mkoa wa Kagera amesema hakutakuwa na Kiingilio na Senene zitakuwepo.

Pia amewakaribisha watanzania wote na kuunga Mkono juhudi zilizoanzishwa na taasisi hiyo ili kufanikisha ndoto za kulijenga taifa.
Wa kwanza Kulia ni Katibu wa maandalizi wa Kagera Dinner part. Kokuhirwa Bagwerwa Matovu akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Juni 11, 2022  wakati wa kuitambulisha  KAGERA DINNER PART itakayofanyika  katika kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam, Juni 24 na 25, 2022 kuanzia saa mbili asubuhi.
Wa pili kutoka Kulia ni Maratibu Mkuu wa Kagera Dinner Part, Ennock Bujuli akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Juni 11, 2022  wakati wa kuitambulisha  KAGERA DINNER PART itakayofanyika  katika kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam, Juni 24 na 25, 2022 kuanzia saa mbili asubuhi. Mweka hazina wa TANUA, Editha Alfred wa kwanza kutoka kushoto,  Makamu Mwenyekiti TANUA, Justinian Kanguru na Mwenyekiti kamati, TANUALeah Rugemalira na wa kwanza kulia ni Katibu wa maandalizi wa Kagera Dinner part. Kokuhirwa Bagwerwa Matovu.
Mwenyekiti kamati TANUA, Leah Rugemalira akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Juni 11, 2022  wakati wa kuitambulisha  KAGERA DINNER PART itakayofanyika  katika kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam, Juni 24 na 25, 2022 kuanzia saa mbili asubuhi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...