Baadhi ya wadau wa utafiti wa umaskini katika mikoa mitano ya Tanzania bara,wameiomba serikali kupunguza umri wa watumishi kustaafu ili kutoa fursa ya ajira kwa vijana wenye elimu mitaani hali inayotajwa kuwa kukosekana kwa ajira kumesababisha ongezeko la umaskini.

Patrick Tweve ni miongoni mwa wadau aliyetoa mapendekezo hayo katika kikao cha uwasilishaji wa matokeo ya utafiti wa kubaini vipimo vipya vya umaskini Tanzania bara uliofanywa kwa miaka mitatu na shirika la kimataifa la ATD.

Hata hivyo miongoni mwa vipimo 13 vya utafiti wa umaskini vilivyobainishwa katika mikoa ya Kigoma,Kilimanjaro,Dodoma,Dar es Salam na Njombe ni pamoja na Mmomonyoko wa maadili,mila na desturi potofu,kilimo kisichokuwa na tija pamoja na mapungufu ya utekelezaji wa sera katika taasisi.

“Tunaomba wapunguze umri wa kustaafu,serikali imeweka miaka 53 mpaka 50 ni afadhari upunguzwe umri ili wenye elimu haha amber wake Mitanni waweze kuajiriwa maana unakuta kuna mfanyakazi ni mzee mpaka akishika peni mikono inatetemeka na wengine waliosoma wanazidi kuwa masikini”alisema Patrick Tweve

Kwa upande wake Abdallah Juma ambaye ni mtafiti mtaalamu katika timu ya utafiti ya Tanzania amesema miongoni mía mapendekezo katika utafiti utafiti wao ni kuiomba serikali kutia mkazo zaidi katika elimi ya ufundi ili jamii iweze kuwa na ujuzi pamoja na maarifa ya kujitegemea.

“Jukumu letu sisi ni kushirikiana na serikali kwasababu huwezi ukafanya utafiti bila kuishirikisha serikali na wao wamechukua matokeo kwa ajili ya kuyafanyia kazi.Lakini pia kwenye utafiti tumetoa mapendekezo yetu tumesema serikali itie mkazo zaidi elimi ya ufundi katika vyuo mbali mbali ili mtu aweze kutoka chuo akiwa na ujuzi”alisema Abdallah Juma
Mtafiti Mtaalamu katika timu ya Utafiti ya Tanzania kupitia shirika la ATD, Abdallah Juma akizungumza namna walivyopata vipimo vipya vya umaskini Tanzania bara kupitia utafiti wao uliofanywa kwa miaka 3 katika mikoa mitano Tanzania bara
Zoezi la utoaji wa utafiti likiendelea katika ukumbi wa Milimani uliopo katika halmashauri ya mji wa Njombe
Baadhi ya wadau wakifuatilia vipimo vya umaskini kupitia utafiti uliofanywa na shirika la ATD

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...