KAMPUNI kinara ya Mafuta nchini TotalEnergies 
imeendelea kuwafikia watanzania wenye malengo ya kumiliki vituo vya 
mafuta kwa kuzindua kituo kipya cha mafuta Kigamboni jijini Dar es 
Salaam, kituo hicho kinamilikiwa na kuendeshwa na mtanzania Mohammed 
Salehe Affif aliyenufaika kupitia programu ya umiliki na uendeshaji 
(DODO) huku ikielezwa kuwa kampuni hiyo itaendelea kutoa huduma bora kwa
 watanzania pamoja na kushirikiana nao katika uwekezaji wa sekta hiyo 
ili kujenga uchumi imara.
Akizungumza
 mara baada ya kuzindua kituo hicho Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni
 James Mkumbo amesema kuwa programu ya DODO inayoendeshwa na kampuni ya 
TotalEnergies ya kushirikiana na wazawa imeleta kituo cha kwanza cha 
mafuta cha TotalEnergies Kigamboni na  kampuni  hiyo ambayo huduma zake 
zinafahamika kwa Umma kupitia ubora wake na viwango vya kimataifa.
''
 Kwa niaba ya wananchi wa Kigamboni na Serikali kwa ujumla niwashukuru 
TotalEnergies kwa kuendelea kuwafikia watanzania kwa kiwango kikubwa cha
 umiliki wa vituo vya mafuta na kushiriki katika kujenga uchumi wa nchi 
kupitia ubunifu, uwekezaji na ajira kupitia vituo hivi.'' Amesema.
Mkumbo
 amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Samia Suluhu 
Hassan ameweka mazingira wezeshi ya uwekezaji yaliyopelekea mwekezaji 
huyo mzawa kufanya uwekezaji mkubwa utakaowanufaisha wananchi wa 
Kigamboni kwa kupata huduma na kutoa ajira kwa vijana wa maeneo jirani.
Aidha
 amempongeza Mohammed Afiff kwa kuwawezesha wananchi wa Kigamboni kiushi
 katika ndoto zao kwa kumiliki kituo kipya cha kisasa kitakachotoa 
huduma kwa wakazi wa kigamboni na maeneo ya karibu na kutoa ajira kwa 
vijana wa maeneo ya jirani.
Amesema
 hiyo ni fursa kwa wananchi na wafanyabiashara wa Kigamboni kupata 
huduma katika kituo hicho kwa kupata huduma za mafuta, kutengeneza 
magari yao pamoja na kupata mahitaji mbalimbali kupitia duka la Bonjour 
linalopatikana ndani ya kituo hicho kwa uhakika na usalama.
Kwa
 upande wake Mkurugenzi wa Biashara wa Vituo vya Mafuta vya 
TotalEnergies Marieme Sav Saw amesema kuwa Wilaya ya Kigamboni imekuwa 
ikikuwa kwa kasi kutokana na juhudi za Serikali za kuweka miundombinu 
wezeshi ya kibiashara inayovutia uwekezaji ikiwemo daraja la Nyerere, 
ujenzi wa barabara kutoka Ferry, Kibada na Kibada hadi Mwasonga hali 
iliyopelekea mzawa huyo kuwekeza kwa manufaa ya wanakigamboni na 
watanzania kwa ujumla.
Marieme
 amesema kuwa mahusiano hayo ni hatua kubwa katika kuendeleza soko la 
mafuta nchini na ni fursa kwa watanzania wenye maeneo na ndoto ya 
kumiliki vituo vya mafuta kuitumia program ya DODO yenye uhakika wa 
soko, mapato pamoja utambuzi kupitia chapa (brand,) ya TotalEnergies 
yenye kutoa huduma bora na salama ikiwemo za mafuta bora (excellium 
fuel) na vilainishi.
Pia
 amesema kuwa ni fahari kwa TotalEnergies kufanya kazi na Mohammed Afiff
 na wanawashukuru wateja wao kwa kuendelea kuwaamini na subira yavuta 
heri kwa sasa wakazi wa Kigamboni watafurahia huduma zenye ubora na 
viwango vya kimataifa.
Kwa
 upande wake mmiliki na mwendeshaji wa kituo hicho Mohammed Afiff  
amesema, amekuwa na ndoto ya kufanya kazi na kampuni ya TotalEnergies 
kutokana na ubora wa huduma wanazozitoa na ubia huo wa kufanikisha 
uzinduzi wa kituo hicho utanufaisha pia wakazi wa maeneo hayo kwa huduma
 za mafuta na vilainishi, bidhaa kupitia duka la Bonjour pamoja na ajira
 kwa wakazi wa maeneo hayo.
Awali
 Meneja wa kuendeleza biashara kwenye vituo Thomas Meitaroni amesema, 
kituo hicho kinachomilikiwa na mtanzania ni matokeo ya programu ya 
umiliki na uendeshaji Dealer Owns, Dealer Operate, (DODO) programu 
iliyobuniwa mahususi kwa wawekezaji wenye maeneo ya kujenga vituo vya 
mafuta vyenye leseni halali zilizotolewa na mamlaka ya Tanzania kuingia 
ubia na na kutumia chapa (brand) ya TotalEnergies.
Amesema
 kupitia DODO wawekezaji wananufaika na kutumia nembo ya TotalEnergies 
kampuni namba moja ya uuzaji mafuta na vilainishi nchini, soko la 
uhakika kote nchini ambako vituo hivyo vimesambaa.
Uzinduzi
 wa  kituo hicho uliambatana na ofa maalum ambapo wateja walipata zawadi
 mbalimbali na kubwa zaidi ni kupata punguzo la shilingi 50 kwa kila 
lita ya mafuta waliyonunua.
Matukio mbalimbali wakati wa hafla ya ufunguzi wa kituo hicho.



.jpeg)







.jpeg)


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...