Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) , Eric Hamissi Leo amekutana na kufanya Mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa (CEO) wa Shirika kubwa la Meli la Linear Messina Duniani lenye makao makuu Italy Ndugu Ignazo Messina katika ofisi za Bandari Jijini Dar es Salaam.
Katika ugeni huo Mkurugenzi wa Messina amemkabidhi tuzo ya ushirikiano Mzuri baina ya TPA na Messina.
Ndugu Ignazo amefurahishwa na utendaji kazi mzuri wa TPA na ameahidi kushirikiana zaidi na TPA MESSINA ili Kuongeza Idadi ya meli zitakozoingia bandari za Tanzania
Kwa upande wake Mkurugenzi wa TPA ndugu ,Eric Hamissi ameahidi kuongeza ushirikiano mzuri na Shirika Hilo ili kuongeza ufanisi katika kuhudumia meli zinazoingia katika Bandari ya Dar es Salaam
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...