Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
Wafanyakazi wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) wamepewa mafunzo ya Mfumo wa e-Mrejesho ambao unaratibu maoni, mapendekezo, maboresho na kupokea malalamiko ili kuboresha utendaji wa kazi wa Bodi na Taasisi mbalimbali za hapa nchini.
Akizungumza wakati wa utoaji mafunzo kwa Wafanyakazi wa Bodi hiyo, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Bodi ya Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Paul Bilabaye amesema Bodi hiyo ipo tayari kuutumia Mfumo huo na kuwahudumia Watanzania ili kuboresha utendaji wao wa kazi zao za kila siku.
“Mfumo huu unatengeneza uwajibikaji wa ndani kwa Mtumishi mmoja mmoja, lakini na Taasisi kwa ujumla, tungetamani tupimwe kwa utekelezaji wa kazi zetu kwa ufanishi na kuwa wasikivu wa maoni ya Wadau kupitia mfumo huu”, amesema Bilabaye.
Ametoa wito kwa wadau wote wa Bodi hiyo, Wanafunzi na Wanachama waliosajiliwa kutoka Sekta za Umma na Sekta binafsi kuwasiliana na Bodi kupitia mfumo huo, pia amewaahidi kutoa utumishi uliotukuka kwa kuhakikisha wanatoa majibu sahihi kwa kila hoja inayotolewa na wadau.
Kwa upande wake, Mkufunzi wa Mafunzo hayo ambaye Meneja TEHAMA, Grace Mselle amesema jamii inaweza kuufikia mfumo huo wa e-Mrejesho kwa njia tatu ambao ni kupitia Tovuti, namna ya pili ni kupitia Simu za mkononi kwa kubonyeza *152*00# na kufuata maelekezo na mwisho kupitia ‘Application’.
Naye, mmoja wa waliopata mafunzo hayo, Shilla Mwandu amesema mafunzo hayo yatawasaidia kuanzia Jamii, Watumishi wa Umma kwa namna ya kutoa malalamiko yao na pongezi kupitia Mfumo huo wa e-Mrejesho.
“Kwetu sisi Watumishi wa Umma ni jambo jema sana, kama kuna sehemu tumekwama, hatujaenda vizuri wawe wazi kutusema na kutuambia ukweli ili tutende kwa uhakika jinsi inavyotakiwa”, amesema Shilla.Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Bodi ya Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Paul Bilabaye akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Bodi hiyo walipomaliza mafunzo ya e-Mrejesho yaliyofanyika katika ofisi za Bodi hiyo jijini Dar es Salaam
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...