WAKAZI waliokuwa wakiishi katika Tarafa Ngorongoro mkoani Arusha na sasa wameamua kuondoka kwa hiyari yao na kwenda kuanza maisha huru katika Kijiji cha Msomela wilayani Handeni mkoani Tanga leo Juni 16,2022 wameanza kuondoka huku wakitimia nafasi hiyo kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwani baada ya kusubiri kwa muda mrefu hatimaye imekuwa.
Mmoja wa wakazi hao kutokana na furaha aliyonayo ameamua kufuta jina la mtoto wake na sasa ameamua kumuita Samia ( jina la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan) na sababu ya kufanya hivyo ni kutoa shukrani yake ya dhati kwa Rais kwa kuamua kuwapa uhakika wa maisha yao na kuwakomboa kuwa huru kwa kuwa na makazi ya kudumu huko wanaokwenda( Msomela).
Wakizungumza leo wakati wakiagana na viongozi wa Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha wakazi hao wamesema hatimaye wanaondoka eneo ambalo limekuwa haliko huru kwao kutokana na Sheria za uhifadhi ambazo hazikutoa nafasi kwao kujiendeleza ikiwa pamoja na kutokuwa na makazi ya kudumu wala kuruhusiwa kujishughulisha na kilikoy na biashara.
Mkazi wa Ngorongoro Paulina Bajuta amesema yeye ni mzaliwa wa Kateshi wilayani Babati lakini ameolewa Ngorongoro na kwa siku ya Leo amefurahi sana na anamshukuru Rais Samia."Nafurahi sana na namshukukuru Rais wetu Samia, nimekubali kwa hiyari yangu sijalazimishwa.Huko tunakokwenda tumeenda kupaona na nimepapenda.
"Nimezunguka kila mahali kwa kweli ni pazuri na nastahili kwasababu kutakuwa huru.Namshukuru sana Rais Samia, sina cha kumpa,sina cha kumwambia lakini naomba niseme kwa upendo huu wa Rais Samia mtoto wangu nimeamua kukata jina lake na sasa anaitwa Samia,",amesema.
Kwa upande wake Beatrice John ambaye ni Mkazi wa Ngorongoro katika Kijiji cha Kimba amesema aamshukuru Mungu kwani amekuwa akiisubiri siku hii siku hii kwa miaka mingi na leo imefika ."Tunaondoka kwa hiyari yetu wenyewe ,tunaenda Mkoa wa Tanga Wilaya ya Handeni Kijiji Cha Msomela , kweli tumefurahi kwasababu tulipokuwa kwenye hifdhi kuna mambo yalitubana.
"Lakini kule tunaenda kupata makazi mapya,tunaenda kushughulika na mifugo, kushughulika na kilimo , biashara ,kweli tumepata fursa nzuri sana.Tunamshukuru mama yetu, Rais wetu Samia Suluhu Hassan , kingine watoto wetu wameenda kupata mambo mengi sana na hii ni fursa kwetu na kile ambacho tumepewa kama fidia zitakwenda kusaidia familia zetu,"amesema.
Wakati huo huo Masiaya Saseka amesema anamshukuru sana Mungu kwa siku ya leo kwa kuwa wamefanikiwa kuhama kutoka Ngorongoro kwenda Handeni kupisha uhifadhi lakini wanawenda kuwa huru."Kwasababu kwenye Hifadhi hatuko sana huru kutokana na Sheria za uhifadhi , tunakwenda kuanza upya, tunamshukuru sana Rais Samia ametuambia ukweli na huu ndio ukweli.
"Tunakwenda kuwa huru kupigania maisha yetu hata watoto tutakaozaa watajua kufanya shughuli nyingine , na watakuwa watu ambao watakuwa na uwezo wa kujitegemea.Tumepata fidia ya nyumba zetu maana wapo wanaopotosha kuhusu hizi fidia lakini niseme tulichopewa ni kazi ya mikono yetu kwa miaka 60, na uhifadhi huu ni kwa ajili ya watoto wetu na kizazi kijacho,"amesema.
Mkazi wa Ngorongoro Paulina Bajuta ambaye yeye ni mzaliwa wa Kateshi wilayani Babati lakini ameolewa Ngorongoro na kwa siku ya leo amefurahi sana na anamshukuru Rais Samia."Nafurahi sana na namshukukuru Rais wetu Samia, nimekubali kwa hiyari yangu sijalazimishwa.Huko tunakokwenda tumeenda kupaona na nimepapenda.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...