Na Said Mwishehe,Michuzi TV

KAMATI ya Wakulima Nyeburu (Chanika) Kata ya Buyuni wilayani Ilala mkoani Dar es Salaam imempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kauli yake ailiyoitoa hivi karibuni kwa kuvihalalisha vijiji zaidi ya 360 vilivyopo pembezoni mwa hifadhi mbalimbali hapa nchini.

Taarifa iliyotolewa na kwa vyombo vya habari leo Juni 14,2022 na Mwenyekiti wa Kamati ya Wakulima Nyeburu Bakari Saidi amesema kauli ya Rais Samia imewafanya viongozi wa kamati ya wakulima Nyeburu wampongeze kwani hata wao ni wa wahanga wa migogoro hityo tangu mwaka 1994 hadi leo hii mwaka 2022 bado wanasumbuliwa.

“Bado tunasumbuliwa licha ya Wizara ya Ardhi kuja kufanya uahakiki ulioshirikisha Wizara ya TAMISEMI , Maliasili na Utalii, TAKUKURU TFS, wakuu wa wilaya ya Ilala na Kisarawe, viongozi wa Serikali za mitaa, mbunge wa jimbo la Ukonga na Kamati ya Wakulima Nyeburu.

“Licha ya kuwepo kwa ramani ya Wizara husika ya Ardhi inayoonesha mipaka halisi lakini bado tunasumbuliwa.Tukijenga tunabomolewa , tukilima na kuotesha mimea wanafyeka.Kulingana na kauli hii inatuonyesha ama kweli Rais wetu ni kiongozi anayejali wanyonge.Tunampongeza sana, Mungu amfanyie wepesi kwa kila jambo,”amesema Said kupitia taarifa hiyo.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...