Njombe
WAKAZI zoezi la uchaguzi mkuu ndani ya Chama cha Mpainduzi (CCM ) ukiendelea kwa ngazi mbalimbali za jumuiya na Chama nchini,Jumuiya ya moja wa wanawake (UWT) imewataka wanawake kuacha mitafaruku na mifarakano baada ya uchaguzi huo.

Agizo hilo limetolewa na mwenyekiti wa UWT Taifa na mjumbe wa kamati kuu Bi.Gaudentia Kabaka wakati akizungumza na wanawake mkoani Njombe alipofanya ziara ya kikazi na kwamba kumekuwapo na viashiria vya mifarakano baina yao ndani ya Chama.

“Tusiwe tumesambaratishana,tumenuniana,tumekosana na tumeachana njioa kuelekea 2025.Kwasababu UWT ni jeshi kubwa hatuwezi kusambaratishana halafu tukaja kushinda”alisema Kabaka

Awali mwenyekiti wa UWT mkoa wa Njombe Scolastika Kevela amesema UWT Mkoa wa Njombe ipo imara katika kuhakikisha jumuiya hiyo na Chama kwa ujumla kinasonga mbele.

“Jumuiya yeti kuna utulhvu na ukiona utulivu huy ujue kuna mwenyewe niwahakikishie kuwa jumuiya yetu tunapendana na kushirikiana huku tukiongozwa na jemedari wetu mkuu mama Samia suluhu Hassan

Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Njombe Ndugu Abdulah Hassan Mwinyi anasema kwa sasa Chama kimesimamisha zoezi la kuwasajili wanachama wapya hadi uchaguzi wa ndani ya Chama utakapokwisha huku Akishindwa kujizuia kueleza mazuri anayoyafanya Rais Samia Suluhu Hassan.

Katibu tawala mkoa wa Njombe Bi.Judica Omary anasema serikali na Chama tawala vina mashirikiano makubwa na ya karibu katika kutekeleza Ilani ya uchaguzi mkuu huku mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa kwa niaba ya mkuu wa mkoa akikiri kuwapo kwa hatua kubwa za maendeleo yanayopigwa mkoani hapo pamoja na kutekeleza kwa kiwango kikubwa maelekezo ya serikali.
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Njombe akizungumza wakati wa kumpokea na kumakaribisha mwenyekiti wao wa UWT taifa bi .Gaudentia Kabaka alipofika mkoani Njombe kwa Zara ya kikazi.
Mwenyekiti wa UWT taifa Gaudentia Kabaka akita amepokea tuzo kwa ajili ya Rais Samia iliyotolewa na waanwake wa mkoa wa Njombe.
Mwenyekiti wa UWT akikagua vikundi via wajasiriamali alipofika katika mkoa wa Njombe kwenye uwanja wa ukumbi wa TURBO mini Njombe alipotembelea mkoani humo kwa ajili ya Zara ya kikazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...