Na Mwandishi Wetu
KWAMUJIBU wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya juu ya hali ya UVIKO 19 nchini visa vya UVIKO 19 vimeongezeka kutoka visa 68 kwa kipindi cha Aprili 2, 2022 hadi Mei 4,2022 mwaka huu na kufikia mpaka visa 161 kwa kipindi cha  Mei 5 hadi Juni 3, 2022.

"Hili ni ongezeko la asilimia 137. katika taarifa yake iliyotolewa na Wizara ya Afya huku imetoa wito kwa wananchi kuendelea kuchukua hatua za kujikinga dhidi ya UVIKO 19 na moja ya hatua hizo ikiwa ni kuchanja chanjo ambazo zinaendelea kutolewa katika vituo maalumu pamoja na Hospitali zote nchini.

Yamesemwa hayo na Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani wa Hospitali ya Rufaa ya Taifa Muhimbili Dkt. Elisha Osati alipofanya mahojiano maalumu na kituo cha AMREF Health Africa Tanzania

Katika kuchangia jitihada hizo za kuhakikisha kuwa watanzania wanachukua hatua sahihi za kujikinga dhidi ya ugonjwa hatari wa Korona Amref Health Afrika Tanzania imeendelea kutoa elimu kote nchini kupitia mitandao ya kijamii pamoja na vyombo vingine vya habari.

Katika moja ya mahojiano ambayo Amref walifanya na Daktari bingwa wa magonjwa ya ndani kutoka Hospitali ya Rufaa ya taifa Muhimbili Dkt. Elisha Osati suala la kukamilisha dozi ya chanjo lilionekana kuwa moja ya mambo muhimu yanayopaswa kuzingatiwa hasa katika kipindi hiki ambacho visa vya UVIKO 19 vimeonekana kuongezeka.

Dkt. Osati alisema kuwa kwa chanjo zote ambazo mtu anahitaji kuchoma zaidi ya mara moja ili kukamilisha dozi basi kinga itakuwa haijakamilika kama mtu huyo hatokamilisha dozi yake.

Kwa namna utaratibu wa chanjo ulivyo mtu akishapata chanjo ya kwanza atapewa tarehe ambayo anatakiwa kurudi kuchoma chanjo ya pili ili kukamilisha dozi. Watu wengi wamekuwa wakishindwa kukamilisha dozi aidha kwa kupuuzia au kukosa nafasi na wapo ambao wameshindwa kwa kukosa taarifa sahihi.

Dkt. Osati anasema sio lazima kurudi katika kituo kile kile ulichopata chanjo ya kwanza ili kukamilisha dozi, inawezekana ukawa umesafiri au umehama na hivyo kujikuta katika eneo tofauti na ulilokuwa mwanzo. Kwa namna mfumo wa chanjo unavyofanya kazi unakuruhusu kupata chanjo yako ya pili popote pale Tanzania katika wakati ambao umeelekezwa na wataalamu wa afya.

Kwa mujibu wa Dkt. Osati mtu ambaye hajakamilisha dozi hana tofauti na mtu ambaye bado hajachanja, hawa wote wapo katika hatari ya kupata ugonjwa mkali endapo wataugua korona. Hivyo ili kupata kinga iliyo kamili dhidi ya korona ni vema kukamilisha dozi lakini pia kufuata mbinu nyingine za kujikinga kama ambavyo zimeelekezwa na wataalamu wa afya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...