Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema Serikali imezingatia vyema suala la Haki za Binadamu kwa wakazi waliokuwa wanaishi Ngorongoro kisha kuamua kuanza kuondoka kwa hiyari yao kuelekea Kijiji Cha Msomera wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.

Dkt. Ndumbaro ameyasema hayo kwenye kikao na wadau wa Haki za Binadamu pamoja na Wakuu wa Mikoa ya Arusha na Tanga, Mhe. John Mongella na Mhe. Adam Malima, leo tarehe 21 Juni, 2022.

"Serikali imezingatia vyema haki za binadamu, imewajengea nyumba wananchi walioamua kuhama kwa hiyari, imewapa maeneo yasiyopungua hekari 3 kila mmoja, imewasafirisha wao na mizigo yao na mifugo wanayomiliki, lakini pia Serikali imewalipa fidia, ". 
Waziri Ndumbaro alisema imekuwa ni muhimu wadau wa Haki za Binadamu kukutana na kujadili suala la Ngorongoro na Loliondo ili kuhakikisha haki za binadamu zinazingatiwa na kujibu hoja zisizo za kweli zinazosambaa kwa haraka katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

Awali, Dkt. Ndumbaro alitoa wasilisho katika kikao na Mabalozi kutoka nchi mbalimbali na taasisi za kimataifa, liloonesha jinsi Serikali inavyozingatia haki na malengo yake kuboresha hali ya watanzania wa maeneo ya Ngorongoro na Loliondo.

Waziri Ndumbaro alisema kwa upande wa Loliondo, Serikali imewapa wananchi zaidi ya asilimia 62 ya eneo la hifadhi ya Loliondo ili kukidhi mahitaji ya wakazi wa sasa na imebakiwa na kiasi cha Kilomita za mraba 1500 kutoka 4000 za awali.

Mawasilisho ya wataalam yameonesha umuhimu wa kuhifadhi maeneo ya Loliondo na Ngorongoro kutokana na sababu za kimazingira na Ikolojia.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...