Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyika Tanzania (CPB), Dkt. Anselim Moshi  akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya Kimataifa ya Kibiashara ya 46 yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya J.K.Nyerere Maarufu kama Sabasaba jijini Dar Es Salaam leo, Julai 7, 2022 
Wananchi wakinunua Nafaka na mafuta katika banda la Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyika Tanzania (CPB) katika katika Maonesho ya Kimataifa ya Kibiashara ya 46 yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya J.K.Nyerere Maarufu kama Sabasaba jijini Dar Es Salaam leo, Julai 7, 2022 

Wananchi wakiangalia Nafaka  katika banda la Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyika Tanzania (CPB) katika katika Maonesho ya Kimataifa ya Kibiashara ya 46 yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya J.K.Nyerere Maarufu kama Sabasaba jijini Dar Es Salaam leo, Julai 7, 2022 

ILI kuhakikisha wakulima wanalima kilimo chenye tija nchini, Serikali kupitia Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko Tanzania (CPB) inaendelea kujenga viwanda katika mikoa yote nchini ili wakulima wawe na soko la uhakika la mazao wanayoyalima.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyika Tanzania (CPB), Dkt. Anselim Moshi wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya Kimataifa ya Kibiashara ya 46 yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya J.K.Nyerere Maarufu kama Sabasaba jijini Dar Es Salaam leo, Julai 7, 2022 amesema kuwa wameshajenga Viwanda katika kanda tano za Tanzania ambapo kila Kanda inaviwanda vya kuchakata Mazao.

Amesema wameunda nchi katika Kanda tano ambazo ni Kanda ya Mashariki inayojumuisha Mikoa ya Morogoro, Pwani, Dar Es Salaam, Lindi na Mtwara. Katika kanda hizi kuna viwanda Dar es Salaam katika maeneo ya Mwenge, Mlimani City, Mwananyamala, Ubungo ambapo wana viwanda na maduka ya kuuza bidhaa za nafaka na mazao Mchanganyiko kwa bei ya Jumla.

Pia wanamaduka katika maeneo ya Mbagala, Gongo la Mboto, Tegeta ili kila mwananchi afikiwe na bidhaa hizo.

Kanda ya kati inayojumuisha mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora, Kigoma na Katavi. Dodoma wanaviwanda viwili kimoja cha kuzalisha Unga wa Mahindi na kiwanda cha kuchakata mbegu za alizeti.

Kanda ya ziwa inajumuisha mikoa ya Mwanza, Mara, Kagera, Simiyu, Geita na Shinyanga. Mwanza wanakiwanda cha kukoboa Mpunga wanasambaza mikoa mingine na kuuza nje ya nchi kama Burundi, Rwanda, Kenya na Uganda.

Kanda ya Nyanda Za juu Kusini, inajumuisha Mikoa ya Iringa, Njombe, Songwe, Mbeya, Rukwa na Ruvuma. Iringa kuna kiwanda cha kusindika Unga wa Mahindi huku Kyera wakiwa waneanza kujenzi wa kujenga kiwanda cha kukoboa mpunga.

Kanda ya Kaskazini inayojumuisha mikoa ya Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga. Katika Mkoa wa Arusha wanaviwanda viwili ambavyo ni kiwanda cha ngano kinachochakata tani 100 kwa siku.

Lakini pia tunakiwanda cha kukoboa mahindi kinauwezo wa kuchakata tani 60 kwa siku. Na bidhaa zake zinauzwa nje ya nchi hasa Kenya pia wanasafirisha nchi ya Kongo na Sudani ya Kusini.

Amesema kuwa Serikali kupitia bodi ya CPB wanampango wa kuhakikisha kwenye upande wa mazao yote ya Nafaka na Mchanganyiko wakulima wanalima kwa kilimo cha Mkataba ili mkulima anakuwa na uhakika mauzo yamazao yake kwa kuweka utaratibu wa Mkataba.

Amesema kuwa Zaidi ya wakulima 6000 wanamikataba ya kilimo hasa Kilimo cha Ngano, Alizeti na kilimo cha Maharage ya Soya.

"Tangia Mwaka juzi (2020) tumeanza mikakati ya kilimo cha Mkataba kuhakikisha tunafanya uhamasishaji ili kuhakikisha kwamba wakulima wanalima kwa mikataba lakini wizara ya kilimo inayomikakati kuhakikisha kwamba wakulima wanapata mbolea, wanapata pembejeo kwa wakati pia wanahamasishwa turudi kwenye miaka ya nyuma ambapo Nchi ilikuwa inazalisha ngano nyingi." Amesema Dkt. Moshi

Amesema Mikataba hiyo inasainiwa na taasisi za kibenki, Mkulima, Wasambazaji Pembejeo na bima pamoja na bodi ya CPB ikiwa ndio Mnunuzi mkuu.

"Kwa mfumo huo wa Mkataba tunaweza kupata kilimo ambacho ni cha Tija." Amesema Dkt.Moshi

"Tumeanzisha kilimo cha mkataba katika Mikoa ya Kasikazini Kilimanjaro Siha, Arusha Monduli, Karatu, Simanjiro na Mkoa wa ManyaraHanang'. Kule kote tumeingia mikataba na wakulima wa ngano, lakini pia tunafanya mkataba kwenye maharage ya Soya na tumeshaanza kwenye mkoa wa Songea.

Pia tumeshaanza mikataba kwenye zao la Alizeti kwenye mikoa ya Singida, Dodoma na Simiyu." Amesema Dkt. Moshi

Amesema kuwa viwanda hivyo vitamsaidia Mkulima kuwa na soko la uhakika na vinatoa ajira kwa vijana, pia kuongezea thamani mazao yanayolimwa hapa nchini ili kuweza kuuza kwenye masoko ya kimataifa na kupata faida zaidi.

Amesema Dhamira ya CPB ni kuhakikisha kwamba Mkulima mdogo mdogo nchini anapata bei shindani katika mazao yake.Aidha bodi imejenga uwezo mkubwa wa kuweza kununua mazao ya mkulima na kufanya uchambuzi kujua mkulima anatumia gharama zipi shambani kwa kufanya hivyo mkulima anahamasika kuendelea kulima zaidi na hii inahakikisha kwamba salama wa Chakula unakuwepo.

Amesema serikali imetoa maelekezo kwa bodi hiyo kuhakikisha kuwa ngano inazalishwa hapa nchini hadi kufikia tani milioni moja na zaidi ifikapo 2025.

Amesema katika kutekeleza mkakati huo mwaka 2021 waliagiza Mbegu za tani 210 Nchini Zambia na kuzigawa kwa wakulima kwa mkopo katika kanda ya Kaskazini na matokeo yalikuwa mazuri.

Amesema kuwa Mwaka huu wamejipanga kwasababu kuna mbegu zimezalishwa ndani ya nchi na serikali imeweka jitihada kupitia taasisi za Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) na Kampuni ya kuzalisha mbegu ya ASA ili kuweza kuzalisha mbegu nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...