Na.Khadija Seif, Michuzi Tv
WADAU wa kazi za Sanaa wajitokeza kutoa maoni na mapendekezo ya namna bora ya Kuratibu Hakimiliki nchini Ili mchakato wa kutoa Mirabaha Kwa wasanii bila upendeleo mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Diamond jubilee Jijini Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wanahabari mara baada ya kufungua mkutano huo Mwenyekiti wa Kamati ya Kuratibu namna bora ya kusimamia Hakimiliki nchini Victor Tesha amesema Serikali Ina lengo la Sanaa zote nchini kuwa ni sehemu ya kubadilisha maisha ya watu hivyo Kwa kupitia mchakato wa awali umeona Bora kuunda kamati itakayoweza kukusanya maoni Kwa wadau wa Sanaa namna gani kazi zao zitawapa vipato vizuri .
Hata hivyo Tesha ametolea ufafanuzi zaidi kuwa Kamati hiyo imeshapokea maoni kutoka Kanda 5 ambapo ni Kanda ya kaskazini,juu,kati na Kanda juu kusini ,Dodoma pamoja na Dar es salaam ambapo umekua Mkoa wa mwisho kufanya tamati ya Makusanyo ya maoni Kwa njia ya ana kwa ana .
"Mikoa yote ilitupa ushirikiano na wadau walijitokeza kwa wingi kuwasilisha maoni yao tofauti na Mkoa wa Dar es salaam pengine kutokana na changamoto za kimajumukumu imekua ngumu Kwa wasanii kujitokeza Kwa wingi ila ipo njia ambayo kwa wasiohudhuria njia ya ana Kwa ana wanaweza kuingia Mtandaoni na kutuma maoni yao."
Pia Tesha amesema Kwa sasa Mfumo huo utadumu Kwa takribani wiki mbili Ili waweze kufanya mchakato wa kuwasilisha mchakato mzima (Cosota).
Kwa upande wa Mjumbe wa Kamati hiyo ya Kuratibu namna bora ya kusimamia Hakimiliki nchini Khamis Mwinyijuma (FA) ameeleza kuwa hakuna changamoto yoyote iliyojitokeza kutokana na wasani wa Bongofleva kutojitokeza kuwasilisha maoni yao kwani yeye ni mmoja ya Msanii ambae yupo Kwa ajili yao na kuhakikisha anawapa taarifa kwa kadri inavotakikana.
"Kwa wadau wote wabunifu ni fursa hii ni kubwa sana kwetu toeni maoni Ili kuboresha usimamizi wa hakimiliki nchi na muweze kunufaika,Serikali ya awamu ya sita ya Mheshimiwa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuhakikisha Kila Mbunifu ananufaika na kazi yake kwahiyo nikiwa kama mjumbe nitahakikisha naendelea kutoa elimu Kwa namna gani Mirabaha inabadilisha maisha ya wasanii Kwa mlengo wa kuwanifaisha na kuona Sanaa ina kipato ."
Hata hivyo ametoa rai Kwa wadau kuendelea kutoa ushirikiano wa kuwasilisha maoni yao kupitia njia ya Mitandao ya kijamii Ili kujaza madodoso yao kufanikisha mchakato wa Kuratibu namna bora ya kusimamia Hakimiliki.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kuratibu ukusanyaji wa maoni ya namna bora ya kusimamia Hakimiliki nchini Victor Tesha akizungumza katika ukumbi wa Diamond jubilee Jijini Dar es salaam na wadau wa Sanaa na kusisitiza kuwa Kamati bado itaendelea kukusanya maoni Kwa njia ya Mtandao Kwa kutuma ujumbe Whatsapp au kujaza dodoso mtandaoniWajumbe wa Kamati ya Kuratibu namna bora ya kusimamia Hakimiliki nchini P funk Majani pamoja na Mwana FA wakizungumza na Msanii wa Taarab Mzee yusuf katika mkutano wa kutoa maoni ya namna bora ya Kuratibu Hakimiliki nchini uliofanyika katika ukumbi wa Diamond jubilee Jijini Dar es salaam
Wadau mbalimbali waliojitokeza katika mkutano wa Kuratibu namna bora ya kusimamia Hakimiliki nchini na kutoa Mirabaha bila upendeleo Kwa Wasanii nchini
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...