MKUU wa Mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Juma Zuberi Homera amesema uwepo wa Kampuni za gesi za TOL Gases unakwenda kuongeza kasi ya uwekezaji katika Mkoa wa Mbeya.

Mheshimiwa Homera ameyasema hayo mara baada ya kupokea taarifa ya Kampuni hiyo kuhusu uwekaji wa mtambo mpya wa gesi ya carbon dioxide katika eneo la Ikama wilayani Rungwe. kutoka katika Kampuni hiyo

Akizungumza mbele ya wanahabari Ofisini kwake jijini Mbeya Homera ameitaja Kampuni ya TOL Gases kuwa inaendelea kuongeza uchumi wa Mkoa na kwamba kiwango kikubwa cha gesi hiyo kinapatikana ndani ya Mkoa wa Mbeya.

“Uwepo wa Kampuni ya TOL Gases kwenye maonesho ya nanenane kitaifa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ndani ya viwanja cha John Mwakangale,imechagiza vizuri kuonesha uwekezaji unavyopiga kasi mkoani Mbeya’’,alisema.

Hata hivyo ametoa rai kwa kampuni ya TOL Gases na kampuni nyingine kushiriki katika maonesho ya nanenane mwaka huu ili kuonesha uwekezaji mkubwa unaofanyika mkoani Mbeya.

Amesisitiza kuendelea kuongezeka kwa Kampuni kubwa mkoani Mbeya zikiwemo kampuni za kukamua mafuta ya palachichi na kampuni kubwa za uvunaji wa gesi ya Carbon dioxide kwenye eneo la Ikama wilaya ya Rungwe ni dalili njema ya Mkoa huo kusonga mbele.

Kampuni ya TOL Gases iliyoanzishwa miaka Zaidi ya 70 inamilikiwa na watanzania wapatao 10,711 kupitia soko la Hisa la Dar es salaam na inajihusisha na uzalishaji wa gesi za viwandani na hospitalini.

Kampuni hiyo kupitia kiwanda chake cha carbon dioxide inahudumia viwanda mbalimbali hapa nchini hivyo kuchochea ukuaji wa viwanda,hasa viwanda vya vinywaji baridi.

Kulingana na taarifa ya kampuni hiyo,pia gesi hiyo inauzwa nchi za nje kama vile Congo DRC,Zimbabwe,Zambia,Malawi na Burundi.

Kampuni ya TOL Gases Julai 29 mwaka huu inatarajia kuweka mtambo mpya wa gesi ya carbon dioxide katika eneo la Ikama wilayani Rungwe.

Mtambo huo mpya utapoanza uzalishaji utaongeza kodi za serikali(Mrabaha),kodi ya mapato, ushuru wa Halmashauri na kuongeza mauzo ya nje hivyo kuongeza fedha za kigeni.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari,Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Julai 28,2022

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...