*Akutana na zaidi ya wastaafu 1000, wenyewe waridhishwa na utaratibu unaotumika kuwasikiliza
Na MWANDISHI WETU
Maelfu
ya wastaafu Mkoani Dar es Salaam wajitokeza kwa wingi katika mkutano wa
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu, Mhe. Profesa Joyce Ndalichako wa kuwasikiliza na kutatua
changamoto mbalimbali zinazowakabili wastaafu.
Waziri
Profesa Ndalichako leo tarehe 22 Julai, 2022 alikutana na baadhi ya
wastaafu wa Mkoa wa Dar es Salaam ikiwa ni muendelezo wa kukutana na
wastaafu kwenye mikoa mbalimbali nchini kwa lengo la kuwasikiliza na
kutatua changamoto zao mbalimbali ambapo mkutano huo ulianza juzi Mkoani
Dodoma.
"Tayari
kama mnavyoona kazi imeanza tunawasikiliza na tunatatua changamoto na
kama nilivyosema Wizara yangu pamoja na mambo mengine ina dhamana ya
kusimamia wastaafu wanaolipwa mafao kupitia Mfuko wa NSSF na PSSSF,"
alisema.
Waziri
Ndalichako alisema hayo leo wakati alipokutana na wastaafu zaidi ya 1,
000 wa Mkoa wa Dar es Salaam ambao wanahudumiwa na Mifuko ya Hifadhi ya
Jamii ya NSSF na PSSSF.
Aidha
alisema anatambua kuwa wapo wastaafu ambao wanalipwa mafao yao kupitia
Hazina kuwa wakifika katika mkutano huo kuna fomu watapewa kwa ajili ya
kuzijaza na baadaye fomu hizo zitawasilishwa Wizara ya Fedha na Mipango.
"Tunao uwezo wa kutatua changamoto moja kwa moja za wastaafu ambao wanalipwa kupitia Mfuko wa NSSF na PSSSF," alisema.
Waziri
Profesa Ndalichako alisema anathamini mchango mkubwa uliotolewa na
wazee katika ujenzi wa Taifa hivyo atahakikisha kwa kushirikiana na
watendaji wa NSSF na PSSSF changamoto zao zinasikilizwa, kutatuliwa na
kupatiwa ufumbuzi.
Alisema
miongoni mwa changamoto za wastaafu aliokutana nao ni pamoja na mapunjo
ya mafao na huku akisisitiza kuwa changamoto zote zitapatiwa ufumbuzi
na kila mstaafu atapata huduma anayostahiki.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu
Mhe. Profesa Joyce Ndalichako akiwasikiliza na kuwahudumia wastaafu
waliojitokeza kwa wingi katika mkutano wake wenye lengo la kusikiliza na
kutatua kero mbalimbali za wastaafu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Mamia
ya wastaafu wa Mkoa wa Dar es Salaam wakisubiri kuhudumiwa wakati wa
mkutano wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na
Wenye Ulemavu, Mhe. Profesa Joyce Ndalichako
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...